Joshua 6:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha wakaangamiza kila kitu mjini humo na kuwaua kwa upanga: Wanaume na wanawake, vijana na wazee, ng'ombe, kondoo na punda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakauweka mji wakfu kwa Mwenyezi Mungu, na kila chenye uhai ndani yake walikiangamiza kwa upanga: wanaume na wanawake, vijana kwa wazee, ng’ombe, kondoo na punda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee, na ng'ombe, na kondoo, na punda, kwa makali ya upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha wakaangamiza kila kitu mjini humo na kuwaua kwa upanga: wanaume na wanawake, vijana na wazee, ng'ombe, kondoo na punda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakauweka mji wakfu kwa BWANA, na kila chenye uhai ndani yake walikiangamiza kwa upanga, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, ng'ombe, kondoo na punda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakauweka mji wakfu kwa bwana, na kila chenye uhai ndani yake walikiangamiza kwa upanga, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, ng’ombe, kondoo na punda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume, wanawake, watoto na wazee, na ng'ombe, kondoo na punda, kwa upanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha wakaangamiza kila kitu mjini humo na kuwaua kwa upanga: Wanaume na wanawake, vijana na wazee, ng'ombe, kondoo na punda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote waliokuwamo mjini wakawatia mwiko wa kuwapo, wakawaua kwa ukali wa panga, waume kwa wake, watoto kwa wazee, hata ng'ombe na kondoo na punda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee, na ng’ombe, na kondoo, na punda, kwa makali ya upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wakaangamiza kila kitu katika muji ule na kuwaua kwa upanga: wanaume na wanawake, vijana na wazee, ngombe, kondoo na punda.