Joshua 6:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoshua akawaambia wale wapelelezi wawili walioipeleleza nchi hiyo, “Nendeni katika nyumba ya yule kahaba; mkamlete yule mwanamke na wale wote ambao ni ndugu zake kama mlivyomwapia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoshua akawaambia wale watu wawili waliokuwa wameipeleleza nchi, “Nendeni nyumbani mwa yule kahaba; mleteni pamoja na wote walio nyumbani mwake, kulingana na kiapo chenu kwake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoshua akawaambia wale wapelelezi wawili walioipeleleza nchi hiyo, “Nendeni katika nyumba ya yule kahaba; mkamlete yule mwanamke na wale wote ambao ni ndugu zake kama mlivyomwapia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoshua akawaambia wale watu wawili waliokuwa wameipeleleza nchi, “Nendeni nyumbani kwa yule kahaba, mleteni pamoja na wote waliomo nyumbani mwake, kulingana na kiapo chenu kwake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoshua akawaambia wale watu wawili waliokuwa wameipeleleza nchi, “Nendeni nyumbani kwa yule kahaba, mleteni pamoja na wote waliomo nyumbani mwake, kulingana na kiapo chenu kwake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoshua akawaambia wale wapelelezi wawili walioipeleleza nchi hiyo, “Nendeni katika nyumba ya yule kahaba; mkamlete yule mwanamke na wale wote ambao ni ndugu zake kama mlivyomwapia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale watu wawili walioipeleleza nchi hiyo Yosua akawaambia: Ingieni nyumbani mwake yule mwanamke mgoni, mmtoe mle nyumbani yule mwanamke nao wote waliomo mwake, kama mlivyomwapia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoshua akawaambia wale wapelelezi wawili walioipeleleza inchi hiyo: “Muende katika nyumba ya yule kahaba; mumulete yule mwanamuke na wale wote ambao ni wandugu zake kama mulivyomwapia.”