Joshua 6:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, wakauchoma moto mji wa Yeriko na kila kitu kilichokuwako isipokuwa fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na vya chuma; hivyo viliwekwa katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wakauchoma mji wote na kila kitu kilichokuwa ndani yake. Lakini fedha, dhahabu, na vyombo vya shaba na vya chuma wakaviweka katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, wakauchoma moto mji wa Yeriko na kila kitu kilichokuwako isipokuwa fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na vya chuma; hivyo viliwekwa katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wakauchoma mji wote na kila kitu kilichokuwamo ndani yake. Lakini fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na chuma wakaviweka katika hazina ya nyumba ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wakauchoma mji wote na kila kitu kilichokuwamo ndani yake. Lakini fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na vya chuma wakaviweka katika hazina ya nyumba ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, wakauchoma moto mji wa Yeriko na kila kitu kilichokuwako isipokuwa fedha, dhahabu, vyombo vya shaba na vya chuma; hivyo viliwekwa katika hazina ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha huo mji wakauteketeza kwa moto pamoja navyo vyote vilivyokuwamo, lakini fedha na dhahabu na vyombo vya shaba na vya chuma wakavitia katika kilimbiko cha Nyumbani mwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, wakauchoma kwa moto muji wa Yeriko na kila kitu kilichokuwa mule isipokuwa feza, zahabu, vyombo vya shaba na vya chuma; hivyo viliwekwa katika hazina ya nyumba ya Yawe.