Joshua 6:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo Yoshua alitamka apizo rasmi mbele ya watu akisema, “Atakayeujenga tena mji wa Yeriko, na alaaniwe na Mungu, Yeyote atakayeweka msingi wa mji huo, mzaliwa wake wa kwanza na afe. Yeyote atakayejenga lango la mji huo, mwanawe kitinda mimba na afe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Na alaaniwe mbele za Mwenyezi Mungu mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko: “Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume ataiweka misingi yake; kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho atayaweka malango yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo Yoshua alitamka apizo rasmi mbele ya watu akisema, “Atakayeujenga tena mji wa Yeriko, na alaaniwe na Mungu, Yeyote atakayeweka msingi wa mji huo, mzaliwa wake wa kwanza na afe. Yeyote atakayejenga lango la mji huo, mwanawe kitinda mimba na afe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Alaaniwe mbele za BWANA mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko: “Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume ataweka misingi yake; kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho ataweka malango yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Aliyelaaniwa mbele za bwana ni mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko: “Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume ataiweka misingi yake; kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho atayaweka malango yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe na BWANA mtu yule atakayeinuka na kutaka kuujenga tena mji huu wa Yeriko; atakayeweka msingi wake mzaliwa wake wa kwanza na afe. Tena atakayesimamisha malango yake mtoto wake wa kiume aliye mdogo na afe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo Yoshua alitamka apizo rasmi mbele ya watu akisema, “Atakayeujenga tena mji wa Yeriko, na alaaniwe na Mungu, Yeyote atakayeweka msingi wa mji huo, mzaliwa wake wa kwanza na afe. Yeyote atakayejenga lango la mji huo, mwanawe kitinda mimba na afe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosua akawaapisha watu hao kwamba: Mtu na awe ameapizwa machoni pa Bwana atakayeinuka, aujenge tena mji huu wa Yeriko! Atakapoweka misingi yake, mwanawe we kwanza atakufa, tena atakapoyatia malango yake, mwanawe mdogo atakufa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za BWANA mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule Yoshua akaapa mbele ya watu akisema: “Atakayeujenga tena muji wa Yeriko, alaaniwe na Mungu. Yeyote atakayeweka musingi wa muji huo, muzaliwa wake wa kwanza akufe. Yeyote atakayejenga mulango wa muji huo, mwana wake kitenda mimba akufe.”