Joshua 6:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulingana na amri ya Yoshua, wale makuhani saba waliokuwa na mabaragumu saba ya kondoo dume wakaenda mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakiwa wanapiga mabaragumu, nyuma yao wakifuatwa na lile sanduku la agano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Yoshua kuzungumza na watu, wale makuhani saba waliozibeba zile baragumu saba mbele za Mwenyezi Mungu, wakatangulia mbele, wakipiga baragumu zao na Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu likawafuata.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele za Bwana, wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la agano la Bwana likawafuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulingana na amri ya Yoshua, wale makuhani saba waliokuwa na mabaragumu saba ya kondoo dume wakaenda mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakiwa wanapiga mabaragumu, nyuma yao wakifuatwa na lile sanduku la agano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Yoshua kuzungumza na watu, wale makuhani saba wenye kuzibeba zile baragumu saba mbele za BWANA, wakatangulia mbele, wakipiga baragumu zao na Sanduku la Agano la BWANA likawafuata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Yoshua kuzungumza na watu, wale makuhani saba wenye kuzibeba zile baragumu saba mbele za bwana, wakatangulia mbele, wakipiga baragumu zao na Sanduku la Agano la bwana likawafuata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua baragumu saba za pembe za kondoo dume mbele za BWANA, watatangulia, wakapiga hayo mabaragumu; nalo sanduku la Agano la BWANA likawafuata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulingana na amri ya Yoshua, wale makuhani saba waliokuwa na mabaragumu saba ya kondoo dume wakaenda mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakiwa wanapiga mabaragumu, nyuma yao wakifuatwa na lile sanduku la agano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yosua alipowaagiza watu hivyo, watambikaji saba wakachukua mabaragumu saba yenye milio mikubwa kwenda mbele ya Bwana, nao wakaenda wakiyapiga hayo mabaragumu, nalo Sanduku la Agano la Bwana likawafuata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele za BWANA, wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la agano la BWANA likawafuata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulingana na amri ya Yoshua, wale makuhani saba waliokuwa na mabaragumu saba ya kondoo dume wakaenda mbele ya Yawe, wakiwa wanapiga mabaragumu, nyuma yao wakifuatwa na lile Sanduku la Agano.