Joshua 7:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wametenda dhambi, maana wamelivunja agano langu nililowaamuru washike; wamevichukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu viangamizwe; wameviiba na kudanganya, wakaviweka pamoja na vitu vyao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa; wameiba, wamesema uongo, na wameviweka pamoja na mali yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wametenda dhambi, maana wamelivunja agano langu nililowaamuru washike; wamevichukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu viangamizwe; wameviiba na kudanganya, wakaviweka pamoja na vitu vyao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka Agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, wameiba, wamesema uongo, wameviweka pamoja na mali zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, wameiba, wamesema uongo, wameviweka pamoja na mali zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wamevificha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli wametenda dhambi, maana wamelivunja agano langu nililowaamuru washike; wamevichukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu viangamizwe; wameviiba na kudanganya, wakaviweka pamoja na vitu vyao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waisiraeli wamekosa wasipolishika agano langu, nililowaagiza, kwa maana wamechukua vitu vyenye mwiko kwa kuviiba, wakavificha na kuvitia katika vyombo vyao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wametenda zambi, maana wamelivunja agano langu nililowaamuru washike. Wametwaa vimoja kati ya vitu vilivyotolewa viangamizwe. Wameviiba na kudanganya, wakaviweka pamoja na vitu vyao.