Joshua 7:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, inuka uwatakase watu, waambie wajitakase na kujitayarisha kwa siku ya kesho, maana mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema hivi: ‘Miongoni mwenu kuna vitu vilivyotolewa viangamizwe; hamwezi kuwakabili adui zenu mpaka vitu hivyo vimeondolewa kati yenu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nenda, ukawatakase watu. Waambie, ‘Jitakaseni mjiandae kwa ajili ya kesho; kwa sababu hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: Vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa vimo kati yenu, ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu hadi mtakapoviondoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, inuka uwatakase watu, waambie wajitakase na kujitayarisha kwa siku ya kesho, maana mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema hivi: ‘Miongoni mwenu kuna vitu vilivyotolewa viangamizwe; hamwezi kuwakabili adui zenu mpaka vitu hivyo vimeondolewa kati yenu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nenda, ukawaweke watu wakfu. Waambie, ‘Jitakaseni mjiandae kwa kesho; kwa sababu hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: Kwamba kitu kilichowekwa wakfu kipo katikati yenu, Ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu mpaka mtakapokiondoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nenda, ukawatakase watu. Waambie, ‘Jitakaseni mjiandae kwa kesho; kwa sababu hili ndilo asemalo bwana, Mungu wa Israeli: Kitu kilichowekwa wakfu kipo katikati yenu, ee Israeli. Hamwezi kusimama dhidi ya adui zenu mpaka mtakapokiondoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, muwe tayari kesho; maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, inuka uwatakase watu, waambie wajitakase na kujitayarisha kwa siku ya kesho, maana mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema hivi: ‘Miongoni mwenu kuna vitu vilivyotolewa viangamizwe; hamwezi kuwakabili adui zenu mpaka vitu hivyo vimeondolewa kati yenu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Inuka, uwaeue hawa watu na kuwaambia: Jieulieni siku ya kesho! Kwani hivyo ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Kiko kiapizo kilichoko katikati yenu, Waisiraeli; kwa hiyo hamtaweza kusimama machoni pa adui zenu, mpaka mkiondoe hicho kiapizo katikati yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, simama uwatakase watu, uwaambie wajitakase na kujitayarisha kwa siku ya kesho, maana mimi Yawe, Mungu wa Israeli, ninasema hivi: ‘Kati yenu kuna vitu vilivyotolewa viangamizwe. Hamuwezi kuwashinda waadui zenu mpaka vitu hivyo vimeondolewa kati yenu!