Joshua 7:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo kesho asubuhi wote mtakuja mbele yangu, kabila baada ya kabila. Kabila nitakalolichagua litakwenda mbele, ukoo baada ya ukoo. Ukoo nitakaouchagua utakwenda mbele, jamaa baada ya jamaa. Na jamaa nitakayoichagua itakwenda mbele, mtu mmojammoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Asubuhi, mtakuja kabila kwa kabila. Kisha kabila atakalolichagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele kufuatana na koo zao; nao ukoo atakaouchagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa atakayoichagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele mtu kwa mtu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa Bwana itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa Bwana itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa Bwana itakaribia mtu kwa mtu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo kesho asubuhi wote mtakuja mbele yangu, kabila baada ya kabila. Kabila nitakalolichagua litakwenda mbele, ukoo baada ya ukoo. Ukoo nitakaouchagua utakwenda mbele, jamaa baada ya jamaa. Na jamaa nitakayoichagua itakwenda mbele, mtu mmojammoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Asubuhi, mjihudhurishe kabila kwa kabila. Itakuwa kabila lile atakalolitwaa BWANA litakuja mbele ukoo kwa ukoo, ukoo ule atakaotwaa BWANA utakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ile atakayoitwaa BWANA itakuja mbele mtu baada ya mtu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Asubuhi, mjihudhurishe kabila kwa kabila. Itakuwa kabila lile atakalolitwaa bwana litakuja mbele ukoo kwa ukoo, ukoo ule atakaoutwaa bwana utakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ile atakayoitwaa bwana itakuja mbele mtu kwa mtu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa BWANA itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa BWANA itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa BWANA itakaribia mtu kwa mtu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo kesho asubuhi wote mtakuja mbele yangu, kabila baada ya kabila. Kabila nitakalolichagua litakwenda mbele, ukoo baada ya ukoo. Ukoo nitakaouchagua utakwenda mbele, jamaa baada ya jamaa. Na jamaa nitakayoichagua itakwenda mbele, mtu mmojammoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho asubuhi sharti mjilete hapa shina kwa shina, nalo shina, Bwana atakalolikamata, litajileta ukoo kwa ukoo, nao ukoo, Bwana atakaoukamata, utajileta mlango kwa mlango, nao mlango, Bwana atakaokamata, watu wake watajileta mmoja mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa BWANA itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa BWANA itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa BWANA itakaribia mtu kwa mtu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo kesho asubui wote mutakuja mbele yangu, kabila kwa kabila. Kabila nitakalolichagua litakwenda mbele, ukoo kwa ukoo. Ukoo nitakaouchagua utakwenda mbele, jamaa kwa jamaa. Na jamaa nitakayoichagua itakwenda mbele, mutu mumoja mumoja.