Joshua 7:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipoona vazi moja zuri kutoka Shinari kati ya nyara, shekeli 200 za fedha na mchi wa dhahabu wenye uzito wa shekeli 50, nikavitamani na kuvichukua; nimevificha ardhini ndani ya hema langu; na fedha iko chini ya vitu hivyo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipoona katika nyara joho zuri la kutoka Babeli, shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu ya uzito wa shekeli hamsini, nikavitamani na nikavichukua. Tazama, vimefichwa ardhini ndani ya hema langu, pamoja na hiyo fedha chini yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipoona vazi moja zuri kutoka Shinari kati ya nyara, shekeli 200 za fedha na mchi wa dhahabu wenye uzito wa shekeli 50, nikavitamani na kuvichukua; nimevificha ardhini ndani ya hema langu; na fedha iko chini ya vitu hivyo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipoona katika nyara joho zuri la kutoka Babeli, shekeli mia mbili za fedha na kabari ya dhahabu uzito wake shekeli hamsini, nikavitamani nami nikavichukua. Tazama, vimefichwa ardhini ndani ya hema langu, pamoja na hiyo fedha chini yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipoona katika nyara joho zuri la kutoka Babeli, shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu ya uzito wa shekeli hamsini, nikavitamani na nikavichukua. Tazama, vimefichwa ardhini ndani ya hema langu, pamoja na hiyo fedha chini yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilipoona katika nyara joho zuri la Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nilivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipoona vazi moja zuri kutoka Shinari kati ya nyara, shekeli 200 za fedha na mchi wa dhahabu wenye uzito wa shekeli 50, nikavitamani na kuvichukua; nimevificha ardhini ndani ya hema langu; na fedha iko chini ya vitu hivyo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipoona katika nyara vazi zuri la Babeli na fedha 200 na ulimi mmoja wa dhahabu wenye uzito wa sekeli 50, ndio ratli mbili, nikaingiwa na tamaa navyo, nikavichukua, viko hemani mwangu, vimefukiwa mchangani, nazo fedha ziko chini yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipoona vazi moja zuri kutoka Sinari kati ya vitu tulivyonyanganya, vikoroti mia mbili vya feza na furushi ya zahabu yenye uzito wa vikoroti makumi tano vya feza, nikavitamani na kuvitwaa; nikavificha katika udongo ndani ya hema langu; na feza iko chini ya vitu hivyo.”