Joshua 7:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoshua pamoja na Waisraeli wote, wakamchukua Akani, mwana wa Zera, pamoja na fedha, vazi, dhahabu, watoto wake wa kiume na binti zake, ng'ombe, punda na kondoo wake, hema lake na kila kitu alichokuwa nacho na kuwapeleka kwenye bonde la Akori.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yoshua, pamoja na Israeli yote, wakamchukua Akani mwana wa Zera, pamoja na ile fedha, lile joho, ile kabari ya dhahabu, wanawe wa kiume na wa kike, ng’ombe, punda na kondoo wake, hema lake pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta katika Bonde la Akori.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng'ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoshua pamoja na Waisraeli wote, wakamchukua Akani, mwana wa Zera, pamoja na fedha, vazi, dhahabu, watoto wake wa kiume na binti zake, ng'ombe, punda na kondoo wake, hema lake na kila kitu alichokuwa nacho na kuwapeleka kwenye bonde la Akori.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yoshua, pamoja na Israeli yote, wakamchukua Akani mwana wa Zera, pamoja na ile fedha, joho, kabari ya dhahabu, wanawe na binti zake, ng'ombe, punda, kondoo, hema pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta katika Bonde la Akori.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Yoshua, pamoja na Israeli yote, wakamchukua Akani mwana wa Zera, pamoja na ile fedha, lile joho, ile kabari ya dhahabu, wanawe na binti zake, ng’ombe, punda na kondoo wake, hema yake pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta katika Bonde la Akori.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng'ombe wake, punda wake na kondoo wake, hema yake na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hadi bonde la Akori.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoshua pamoja na Waisraeli wote, wakamchukua Akani, mwana wa Zera, pamoja na fedha, vazi, dhahabu, watoto wake wa kiume na binti zake, ng'ombe, punda na kondoo wake, hema lake na kila kitu alichokuwa nacho na kuwapeleka kwenye bonde la Akori.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosua akamchukua Akani, mwana ma Zera, pamoja na zile fedha na lile vazi na ule ulimi wa dhahabu, hata wanawe wa kiume na wa kike, na ng'ombe wake na punda wake na mbuzi na kondoo wake na hema lake navyo vyote vilivyokuwa vyake, nao Waisiraeli wote wakaenda naye, wakawapeleka wote katikati ya bonde la Akori.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoshua pamoja na Waisraeli wote, wakamukamata Akana mwana wa Zera, pamoja na feza, nguo, zahabu, watoto wake wa kiume na wabinti zake, ngombe, punda na kondoo wake, hema lake na kila kitu alichokuwa nacho na kuwapeleka kwenye bonde la Akori.