Joshua 7:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoshua akamwuliza Akani, “Kwa nini umetuletea taabu? Mwenyezi-Mungu atakuletea taabu wewe mwenyewe leo.” Waisraeli wote wakampiga Akani kwa mawe mpaka akafa. Kisha wakawapiga jamaa yake yote kwa mawe mpaka wakafa, wakawateketeza wote kwa moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoshua akasema, “Kwa nini umetuletea taabu hii? Mwenyezi Mungu atakuletea taabu leo.” Ndipo Israeli yote ikampiga Akani kwa mawe, na baada ya kuwapiga jamaa yake yote kwa mawe, wakawateketeza kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? Bwana atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoshua akamwuliza Akani, “Kwa nini umetuletea taabu? Mwenyezi-Mungu atakuletea taabu wewe mwenyewe leo.” Waisraeli wote wakampiga Akani kwa mawe mpaka akafa. Kisha wakawapiga jamaa yake yote kwa mawe mpaka wakafa, wakawateketeza wote kwa moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoshua akasema, “Kwa nini umeleta taabu hii juu yetu? BWANA ataleta taabu juu yako leo hii.” Ndipo Waisraeli wote wakampiga Akani kwa mawe, na baada ya kuwapiga jamaa yake yote kwa mawe, wakawateketeza kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoshua akasema, “Kwa nini umeleta taabu hii juu yetu? bwana ataleta taabu juu yako leo hii.” Ndipo Israeli yote ikampiga Akani kwa mawe, na baada ya kuwapiga jamaa yake yote kwa mawe, wakawateketeza kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoshua akamwuliza Akani, “Kwa nini umetuletea taabu? Mwenyezi-Mungu atakuletea taabu wewe mwenyewe leo.” Waisraeli wote wakampiga Akani kwa mawe mpaka akafa. Kisha wakawapiga jamaa yake yote kwa mawe mpaka wakafa, wakawateketeza wote kwa moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko Yosua akasema: Kama ulivyotupatia mabaya, ndivyo Bwana akupatie mabaya nawe siku hii ya leo! Ndipo, Waisiraeli wote walipompiga mawe, navyo vile vitu wakavichoma moto, nao wale watu wakawaua kwa kuwapiga mawe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoshua akamwuliza Akana: “Kwa nini umetuletea taabu? Yawe atakuletea taabu wewe mwenyewe leo.” Waisraeli wote wakamupiga Akana kwa mawe mpaka akakufa. Kisha wakawapiga jamaa yake yote kwa mawe mpaka wakakufa, wakawateketeza wote kwa moto.