Joshua 7:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu wakarundika mawe mengi juu yake, ambayo yako hadi leo. Hapo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikapoa; na mahali hapo pakaitwa Bonde la Akori mpaka hivi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakakusanya lundo la mawe juu ya Akani, ambalo lipo hadi leo. Naye Mwenyezi Mungu akageuka kutoka hasira yake kali. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Bonde la Akori tangu siku hiyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye Bwana akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu wakarundika mawe mengi juu yake, ambayo yako hadi leo. Hapo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikapoa; na mahali hapo pakaitwa Bonde la Akori mpaka hivi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakakusanya lundo la mawe juu ya Akani, ambalo lipo mpaka leo. Naye BWANA akageuka kutoka katika hasira yake kali. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Bonde la Akori tangu siku hiyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakakusanya lundo la mawe juu ya Akani, ambalo lipo mpaka leo. Naye bwana akageuka kutoka hasira yake kali. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Bonde la Akori tangu siku hiyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wakakusanya juu yake rundo kubwa la mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu wakarundika mawe mengi juu yake, ambayo yako hadi leo. Hapo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikapoa; na mahali hapo pakaitwa Bonde la Akori mpaka hivi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa la mawe lililoko mpaka siku hii ya leo. Ndipo, Bwana alipoyaacha makali yake yenye moto. Kwa hiyo wakaliita jina lake mahali pale Bonde la Akori (Bonde la Mabaya) mpaka siku hii ya leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wakalundika mawe mengi juu yake, ambayo yako mpaka leo. Hapo hasira ya Yawe ikapoa; na pahali pale pakaitwa Bonde la Akori, ni kusema Bonde la Taabu, mpaka hivi leo.