Joshua 7:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliporudi, wakamwambia Yoshua, “Hakuna haja kupeleka watu wote kuushambulia mji wa Ai, maana wakazi wake ni wachache tu. Watu elfu mbili au tatu watatosha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliporudi kwa Yoshua, wakasema, “Si lazima watu wote waende kupigana na Ai. Watume watu elfu mbili au tatu wakauteke huo mji. Usiwachoshe watu wote, kwa sababu huko kuna watu wachache tu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, Wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu, wakaupige Ai; usiwataabishe watu wote kwa kuwaendesha huko; maana watu hao ni wachache tu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliporudi, wakamwambia Yoshua, “Hakuna haja kupeleka watu wote kuushambulia mji wa Ai, maana wakazi wake ni wachache tu. Watu elfu mbili au tatu watatosha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliporudi kwa Yoshua, wakasema, “Si lazima watu wote waende kupigana na Ai. Watume watu elfu mbili au tatu wakauteke huo mji. Hakuna sababu ya kuwachosha watu wote, kwa sababu huko kuna watu wachache tu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliporudi kwa Yoshua, wakasema, “Si lazima watu wote waende kupigana na Ai. Watume watu elfu mbili au tatu wakauteke huo mji. Usiwachoshe watu wote, kwa sababu huko kuna watu wachache tu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, Wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu, wakaupige Ai; usiwataabishe watu wote kwenda huko maana watu hao ni wachache tu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliporudi, wakamwambia Yoshua, “Hakuna haja kupeleka watu wote kuushambulia mji wa Ai, maana wakazi wake ni wachache tu. Watu elfu mbili au tatu watatosha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waliporudi kwa Yosua wakamwambia: Wasiende watu wote kupanda huko! Watu kama 2000 au 3000 watatosha, waupige Ai. Usiwasumbue watu wote pia! Kwani wao ni wachache.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, Wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu, wakaupige Ai; usiwataabishe watu wote kwa kuwaendesha huko; maana watu hao ni wachache tu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliporudi, wakamwambia Yoshua: “Hakuna lazima ya kupeleka watu wote kuushambulia muji wa Ai, maana wakaaji wake ni wachache tu. Watu elfu mbili au tatu watatosha.”