Joshua 7:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Ai wakawaua Waisraeli thelathini na sita na kuwafukuza wengine kutoka lango la mji mpaka Shebarimu, wakawaua kwenye mteremko. Waisraeli wakafa moyo na kulegea kama maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ambao waliwaua wanaume kama thelathini na sita miongoni mwao. Wakawafukuza Waisraeli kutoka lango la mji hadi Shebarimu, nao wakawauwa huko kwenye miteremko. Kutokana na hili mioyo ya watu ikayeyuka kwa hofu, ikawa kama maji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Ai wakawaua Waisraeli thelathini na sita na kuwafukuza wengine kutoka lango la mji mpaka Shebarimu, wakawaua kwenye mteremko. Waisraeli wakafa moyo na kulegea kama maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ambao waliwaua watu kama thelathini na sita miongoni mwao. Wakawafukuza Waisraeli kutoka lango la mji hadi Shebarimu, nao wakawapiga huko kwenye matelemko. Kutokana na hili mioyo ya watu ikayeyuka ikawa kama maji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ambao waliwaua watu kama thelathini na sita miongoni mwao. Wakawafukuza Waisraeli kutoka lango la mji hadi Shebarimu, nao wakawauwa huko kwenye materemko. Kutokana na hili mioyo ya watu ikayeyuka ikawa kama maji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye materemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Ai wakawaua Waisraeli thelathini na sita na kuwafukuza wengine kutoka lango la mji mpaka Shebarimu, wakawaua kwenye mteremko. Waisraeli wakafa moyo na kulegea kama maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nao watu wa Ai wakaua kwao kama 36, wakawakimbiza kuanzia kwenye lango la mji mpaka kufika Sebarimu, wakawaua huko penye mtelemko; ndipo, mioyo ya watu ilipoyeyuka kuwa kama maji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Ai wakawaua Waisraeli makumi tatu na sita na kuwafukuza wengine kutoka mulango wa muji mpaka Sebarimu, wakawaua kwenye muteremuko. Waisraeli wakavunjika moyo na kuregea kama maji.