Joshua 7:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoshua akayararua mavazi yake, yeye pamoja na wazee wa Israeli. Wakajitupa chini mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu mpaka jioni; wakajitia mavumbi vichwani mwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu, na akabakia hapo hadi jioni. Wazee wa Israeli nao wakafanya vivyo hivyo, wakatia mavumbi vichwani mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoshua akayararua mavazi yake, yeye pamoja na wazee wa Israeli. Wakajitupa chini mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu mpaka jioni; wakajitia mavumbi vichwani mwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yoshua akararua mavazi yake, akapomoka kifudifudi mbele ya Sanduku la BWANA, akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli wakafanya vivyo hivyo, wakatia mavumbi vichwani mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la bwana, na akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli nao wakafanya vivyo hivyo wakatia mavumbi vichwani mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hadi jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoshua akayararua mavazi yake, yeye pamoja na wazee wa Israeli. Wakajitupa chini mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu mpaka jioni; wakajitia mavumbi vichwani mwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yosua akazirarua nguo zake, akajiangusha chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana mpaka jioni, yeye na wazee wa Waisiraeli, wakitia mavumbi vichwani pao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoshua akapasua nguo yake, yeye pamoja na wazee wa Israeli. Wakajitupa chini ya Sanduku la Yawe mpaka magaribi; wakajitia mavumbi juu ya vichwa vyao.