Joshua 8:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usiwe na wasiwasi wowote; wachukue wanajeshi wako wote uelekee mji wa Ai, kwani mfalme wa Ai nimemtia mikononi mwako, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usivunjike moyo. Chukua jeshi lote la vita uende pamoja nalo kuishambulia Ai. Kwa kuwa nimeshamweka mikononi mwako mfalme wa Ai, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Bwana akamwambia Yoshua, Usiche, wala usifadhaike; wachukue watu wote wa vita waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usiwe na wasiwasi wowote; wachukue wanajeshi wako wote uelekee mji wa Ai, kwani mfalme wa Ai nimemtia mikononi mwako, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo BWANA akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usivunjike moyo, chukua jeshi lote la vita uende pamoja nalo kuishambulia Ai. Kwa kuwa nimeshamweka mikononi mwako huyo mfalme wa Ai, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo bwana akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usivunjike moyo. Chukua jeshi lote la vita uende pamoja nalo kuishambulia Ai. Kwa kuwa nimeshamweka mikononi mwako mfalme wa Ai, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha BWANA akamwambia Yoshua, Usiogope, wala usifadhaike; wachukue askari wako wote waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usiwe na wasiwasi wowote; wachukue wanajeshi wako wote uelekee mji wa Ai, kwani mfalme wa Ai nimemtia mikononi mwako, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Bwana akamwambia Yosua: Usiogope, wala usiingiwe na vituko! Wachukue watu wote kwenda vitani pamoja na wewe! Kisha ondoka kuupandia Ai! Tazama, nimemtia mfalme wa Ai mkononi mwako pamoja na watu wake na mji wake na nchi yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha BWANA akamwambia Yoshua, Usiche, wala usifadhaike; wachukue watu wote wa vita waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akamwambia Yoshua: “Usiogope, wala usikuwe na wasiwasi wowote; uwatwae waaskari wako wote uelekee muji wa Ai, maana nimetia mufalme wa Ai katika mikono yako, pamoja na watu wake, muji wake na inchi yake.