Joshua 8:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakusanya Waisraeli na kuelekea mjini Ai, akiwa pamoja na wazee.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Yoshua akakusanya jeshi lake, na yeye na viongozi wa Israeli wakawaongoza kwenda Ai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakusanya Waisraeli na kuelekea mjini Ai, akiwa pamoja na wazee.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yoshua akaamka asubuhi na mapema siku ya pili, akawakutanisha watu wake, yeye na viongozi wa Israeli wakawa mbele ya watu kwenda Ai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi na mapema siku iliyofuatia, Yoshua akawakutanisha watu wake, na yeye na viongozi wa Israeli wakawa mbele ya watu kwenda Ai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakusanya Waisraeli na kuelekea mjini Ai, akiwa pamoja na wazee.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake Yosua akaamka na mapema, akawakagua watu wake, kisha akapanda yeye pamoja wa wazee wa Waisiraeli na kuwaongoza watu kwenda Ai.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoshua akaamuka asubui mapema, akawakusanya Waisraeli na kuelekea katika muji wa Ai, akiwa pamoja na wazee.