Joshua 8:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanajeshi wote waliofuatana naye walikaribia mji na kupiga kambi kaskazini yake, ngambo ya bonde mkabala wa mji wa Ai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanajeshi wote waliokuwa pamoja na Yoshua walipanda, wakakaribia na kufika mbele ya mji. Wakapiga kambi kaskazini mwa Ai, pakiwa na bonde kati yao na huo mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wote, hao wa vita, waliokuwa pamoja naye, wakaenda wakakaribia, na kufikilia mbele ya mji, wakatua upande wa kaskazini wa Ai; napo palikuwa na bonde kati ya yeye na Ai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanajeshi wote waliofuatana naye walikaribia mji na kupiga kambi kaskazini yake, ng'ambo ya bonde mkabala wa mji wa Ai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda, wakakaribia na kufika mbele ya mji. Wakapiga kambi kaskazini ya Ai, pakiwa na bonde kati yao na huo mji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda, wakakaribia na kufika mbele ya mji. Wakapiga kambi kaskazini mwa Ai, pakiwa na bonde kati yao na huo mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wote, hao wa vita, waliokuwa pamoja naye, wakaenda wakakaribia, na kufika mbele ya mji, wakatua upande wa kaskazini wa Ai; napo palikuwa na bonde kati yao na Ai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanajeshi wote waliofuatana naye walikaribia mji na kupiga kambi kaskazini yake, ngambo ya bonde mkabala wa mji wa Ai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wapiga vita wote waliokuwa naye wakapanda kuukaribia mji; walipofika ng'ambo ya huku ya mji wakalala upande wa kaskazini wa Ai, napo hapo katikati yao na mji wa Ai palikuwa bonde.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wote, hao wa vita, waliokuwa pamoja naye, wakaenda wakakaribia, na kufikilia mbele ya mji, wakatua upande wa kaskazini wa Ai; napo palikuwa na bonde kati ya yeye na Ai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari wote waliofuatana naye walikaribia muji na kupiga kambi upande wake wa kaskazini, ngambo ya bonde kuelekeana na muji wa Ai.