Joshua 8:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtautendea mji wa Ai pamoja na mfalme wake kama vile mlivyoutendea mji wa Yeriko pamoja na mfalme wake. Mali zake pamoja na mifugo yake mtakayoteka itakuwa ni mali yenu. Nendeni mwuvamie mji kutoka upande wa nyuma.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utautendea mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyotendea Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mnaweza kunyakua mali zao na mifugo yao kuwa nyara zenu. Weka waviziaji upande wa nyuma ya mji.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nawe utautenda mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyoutenda mji wa Yeriko na mfalme wake; lakini nyara zake na wanyama wake wa mji mtavitwaa kuwa mateka yenu wenyewe; huo mji uuwekee waoteaji upande wa nyuma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtautendea mji wa Ai pamoja na mfalme wake kama vile mlivyoutendea mji wa Yeriko pamoja na mfalme wake. Mali zake pamoja na mifugo yake mtakayoteka itakuwa ni mali yenu. Nendeni mwuvamie mji kutoka upande wa nyuma.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utafanya Ai na mfalme wake kama ulivyofanya kwa mji wa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mnaweza kuchukua mateka yake na mifugo yake, kwa ajili yenu. Weka waviziaji upande wa nyuma ya mji.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utafanya Ai na mfalme wake kama ulivyofanya kwa mji wa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mnaweza kuchukua mateka wake na mifugo wake, kwa ajili yenu. Weka waviziaji upande wa nyuma ya mji.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nawe utautenda mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyoutenda mji wa Yeriko na mfalme wake; lakini nyara zake na wanyama wake wa mji mtavitwaa kuwa mateka yenu wenyewe; huo mji uuwekee waoteaji upande wa nyuma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtautendea mji wa Ai pamoja na mfalme wake kama vile mlivyoutendea mji wa Yeriko pamoja na mfalme wake. Mali zake pamoja na mifugo yake mtakayoteka itakuwa ni mali yenu. Nendeni mwuvamie mji kutoka upande wa nyuma.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe uufanyizie Ai na mfalme wake, kama ulivyoufanyizia Yeriko na mfalme wake, vitu vyake tu mtakavyoviteka pamoja na nyama wao wa kufuga mtajichukulia, viwe mateka yenu. Jipatie penye kuuvizia mji upande wake wa nyuma!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nawe utautenda mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyoutenda mji wa Yeriko na mfalme wake; lakini nyara zake na wanyama wake wa mji mtavitwaa kuwa mateka yenu wenyewe; huo mji uuwekee waoteaji upande wa nyuma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutautendea muji wa Ai pamoja na mufalme wake kama vile mulivyoutendea muji wa Yeriko pamoja na mufalme wake. Mali zake pamoja na nyama wake mutakayoteka itakuwa ni mali yenu. Muende muushambulie muji kutoka upande wa nyuma.”