Joshua 8:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu waliobaki mjini walitoka, lakini wote wakawa wamezingirwa na Waisraeli; nao wakauawa, asibaki hata mmoja wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale waviziaji nao pia wakatoka nje ya mji dhidi yao, hivi kwamba wakashikiwa katikati, Waisraeli wakiwa pande zote mbili. Israeli wakawaua, bila kuwaachia yeyote aliyenusurika wala aliyetoroka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena hao; wengine wakatoka nje kuutoka huo mji kinyume chao; basi hivyo walikuwa wa katikati ya Israeli, wengine upande huu na wengine upande huu; nao wakawapiga, hata wasimwache hata mmoja miongoni mwao aliyesalia, wala kupona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu waliobaki mjini walitoka, lakini wote wakawa wamezingirwa na Waisraeli; nao wakauawa, asibaki hata mmoja wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waviziaji nao wakatoka nje ya mji dhidi yao kuwashambulia kwa nyuma, hivyo watu wa Ai wakashikiwa katikati, Waisraeli wakiwa pande zote mbili. Israeli wakawaua, bila kuwaachia ye yote aliyenusurika wala aliyetoroka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale waviziaji nao pia wakatoka nje ya mji dhidi yao, hivi kwamba wakashikiwa katikati, Waisraeli wakiwa pande zote mbili. Israeli wakawaua, bila kuwaachia yeyote aliyenusurika wala aliyetoroka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena hao; wengine wakatoka nje ya mji huo kinyume chao; hivyo basi wakawa katikati ya Waisraeli, wengine upande huu na wengine upande ule; nao wakawapiga, hata wasimwache hata mmoja miongoni mwao aliyesalia, wala kupona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu waliobaki mjini walitoka, lakini wote wakawa wamezingirwa na Waisraeli; nao wakauawa, asibaki hata mmoja wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wale wa mjini wakatoka kuwaendea nao; ndivyo, hao walivyokuwa katikati ya Waisiraeli, hawa huku nao wale huko, wakawapiga, wasisaze hata mmoja aliyekimbia na kujiponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena hao; wengine wakatoka nje kuutoka huo mji kinyume chao; basi hivyo walikuwa wa katikati ya Israeli, wengine upande huu na wengine upande huu; nao wakawapiga, hata wasimwache hata mmoja miongoni mwao aliyesalia, wala kupona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu waliobaki katika muji walitoka, lakini wote wakakuwa wamezungukwa na Waisraeli; nao wakauawa, wala hakukubaki hata mumoja wao.