Joshua 8:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kama Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza Waisraeli, kadiri ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Mose kwamba itakuwa madhabahu iliyojengwa kwa mawe ambayo hayakuchongwa, wala kuguswa na chombo chochote cha chuma. Juu ya madhabahu hiyo walimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za kuteketezwa na sadaka za amani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Musa: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea Mwenyezi Mungu sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama Musa, mtumishi wa Bwana, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa Bwana, na kuchinja sadaka za amani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kama Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza Waisraeli, kadiri ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Mose kwamba itakuwa madhabahu iliyojengwa kwa mawe ambayo hayakuchongwa, wala kuguswa na chombo chochote cha chuma. Juu ya madhabahu hiyo walimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za kuteketezwa na sadaka za amani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama Mose mtumishi wa BWANA alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Mose: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea BWANA sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama Musa mtumishi wa bwana alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Musa: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea bwana sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa BWANA, na kuchinja sadaka za amani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kama Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza Waisraeli, kadiri ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Mose kwamba itakuwa madhabahu iliyojengwa kwa mawe ambayo hayakuchongwa, wala kuguswa na chombo chochote cha chuma. Juu ya madhabahu hiyo walimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za kuteketezwa na sadaka za amani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama Mose, mtumishi wa Bwana, alivyowaagiza wana wa Isiraeli, kama vilivyoandikwa katika kitabu cha Maonyo ya Mose, alipajenga pale pa kutambikia kwa mawe mazima yasiyochongwa kwa chuma cha mtu, akamtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, wakachinja hata ng'ombe za tambiko za shukrani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa BWANA, na kuchinja sadaka za amani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kama vile Musa mutumishi wa Yawe alivyowaagiza Waisraeli, kadiri ilivyoandikwa katika kitabu cha Sheria ya Musa kwamba itakuwa mazabahu iliyojengwa kwa mawe ambayo hayakuchongwa, wala kuguswa na chombo chochote cha chuma. Juu ya mazabahu hiyo wakamutolea Yawe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani.