Joshua 8:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli wote pamoja na viongozi wao, wazee na waamuzi na wageni wote waliokuwa kati yao, wakasimama kila upande mkabala na sanduku la agano mbele ya makuhani Walawi waliokuwa wamelibeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu. Nusu yao wakasimama mbele ya mlima Gerizimu na nusu nyingine wakasimama mbele ya mlima Ebali, kama vile Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, alivyoagiza hapo awali kuhusu kubarikiwa kwa Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wote, wakiwa na wazee wao, maafisa na waamuzi, walikuwa wamesimama pande zote mbili za Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu, wakiwaelekea makuhani Walawi waliokuwa wamelibeba. Wageni walioishi miongoni mwao, pamoja na wazawa, walikuwa hapo. Nusu ya watu walisimama mbele ya Mlima Gerizimu, na nusu nyingine wakasimama mbele ya Mlima Ebali, kama vile Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameamuru hapo mwanzo alipotoa maagizo ya kuwabariki watu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Israeli wote, na wazee wao, na maakida yao, na makadhi yao, wakasimama upande huu wa sanduku na upande huu, mbele ya makuhani Walawi, waliolichukua sanduku la agano la Bwana, huyo aliyekuwa mgeni pamoja na huyo mzalia; nusu yao mbele ya mlima Gerizimu, na nusu yao mbele ya mlima Ebali, kama Musa, mtumishi wa Bwana, alivyoamuru, ili wawabarikie watu wa Israeli kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli wote pamoja na viongozi wao, wazee na waamuzi na wageni wote waliokuwa kati yao, wakasimama kila upande mkabala na sanduku la agano mbele ya makuhani Walawi waliokuwa wamelibeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu. Nusu yao wakasimama mbele ya mlima Gerizimu na nusu nyingine wakasimama mbele ya mlima Ebali, kama vile Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, alivyoagiza hapo awali kuhusu kubarikiwa kwa Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Israeli wote, wageni na wazawa sawasawa, wazee wao, maafisa wao na waamuzi, walikuwa wamesimama pande zote mbili za hilo Sanduku la Agano la BWANA, wakiwaelekea wale waliokuwa wamelichukua, yaani makuhani, ambao ni Walawi. Nusu ya watu walisimama mbele ya mlima wa Gerizimu na nusu yao walisimama mbele ya mlima wa Ebali, kama vile Mose mtumishi wa BWANA alivyokuwa amewaagiza hapo mwanzo alipowapa maagizo ili kuwabariki watu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Israeli yote, wageni na wazawa sawasawa, wakiwa na wazee wao, maafisa na waamuzi, walikuwa wamesimama pande zote mbili za Sanduku la Agano la bwana, wakiwaelekea wale waliokuwa wamelichukua, yaani makuhani, ambao ni Walawi. Nusu ya watu ilisimama mbele ya Mlima Gerizimu na nusu hiyo ingine ikasimama mbele ya Mlima Ebali, kama vile Musa mtumishi wa bwana alivyokuwa ameamuru hapo mwanzo alipotoa maagizo ya kuwabariki watu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Israeli wote pamoja na wazee, viongozi wao na waamuzi wao, wakasimama upande huu wa sanduku na upande huu, mbele ya makuhani Walawi, waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, huyo aliyekuwa mgeni pamoja na huyo mzaliwa; nusu yao mbele ya mlima Gerizimu, na nusu yao mbele ya mlima Ebali, kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyoamuru hapo awali, ili wawabariki watu wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli wote pamoja na viongozi wao, wazee na waamuzi na wageni wote waliokuwa kati yao, wakasimama kila upande mkabala na sanduku la agano mbele ya makuhani Walawi waliokuwa wamelibeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu. Nusu yao wakasimama mbele ya mlima Gerizimu na nusu nyingine wakasimama mbele ya mlima Ebali, kama vile Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, alivyoagiza hapo awali kuhusu kubarikiwa kwa Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao Waisiraeli wote, wazee wao na wenye amri na waamuzi wao walikuwa wamesimama huku na huko penye lile Sanduku na kuwaelekea watambikaji Walawi waliolichukua Sanduku la Agano la Bwana, wageni pamoja na wazalia, nusu yao waliuelekea mlima wa Gerizimu, nusu waliuelekea mlima wa Ebali, kama Mose, mtumishi wa Bwana, alivyowaagiza kale kuubariki ukoo wa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Israeli wote, na wazee wao, na maakida yao, na makadhi yao, wakasimama upande huu wa sanduku na upande huu, mbele ya makuhani Walawi, waliolichukua sanduku la agano la BWANA, huyo aliyekuwa mgeni pamoja na huyo mzalia; nusu yao mbele ya mlima Gerizimu, na nusu yao mbele ya mlima Ebali, kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyoamuru, ili wawabarikie watu wa Israeli kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wote pamoja na viongozi wao, wazee na waamuzi na wageni wote waliokuwa kati yao, wakasimama kila upande kuelekeana na Sanduku la Agano mbele ya makuhani Walawi waliokuwa wamelibeba Sanduku la Agano la Yawe. Nusu yao wakasimama mbele ya mulima Gerizimu na nusu nyingine wakasimama mbele ya mulima Ebali, kama vile Musa, mutumishi wa Yawe alivyoagiza pale mbele juu ya kubarikiwa kwa Waisraeli.