Joshua 8:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yoshua akawaambia waende mahali pao pa kuvizia; nao wakajiweka magharibi ya mji wa Ai kati ya mji wa Ai na Betheli. Lakini Yoshua alilala usiku huo katika kambi ya Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yoshua akawatuma watu, nao wakaenda mahali pa kujificha, wakawa wanavizia kati ya Betheli na Ai, kuelekea upande wa magharibi wa Ai, lakini Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hata hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yoshua akawaambia waende mahali pao pa kuvizia; nao wakajiweka magharibi ya mji wa Ai kati ya mji wa Ai na Betheli. Lakini Yoshua alilala usiku huo katika kambi ya Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yoshua akawatuma watu, nao wakaenda mahali pa kujificha, wakawa wanavizia kati ya Betheli na Ai, kuelekea upande wa magharibi wa Ai, lakini Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yoshua akawatuma watu, nao wakaenda mahali pa kujificha, wakawa wanavizia kati ya Betheli na Ai, kuelekea upande wa magharibi wa Ai, lakini Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku huo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hadi hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yoshua akawaambia waende mahali pao pa kuvizia; nao wakajiweka magharibi ya mji wa Ai kati ya mji wa Ai na Betheli. Lakini Yoshua alilala usiku huo katika kambi ya Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosua akawatuma, nao wakaenda mahali pa kuvizia, wakakaa katikati ya Beteli na ya Ai upande wa baharini wa Ai. Naye Yosua akalala usiku huo katikati ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hata hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yoshua akawaambia waende pahali pao pa kuvizia; nao wakajiweka upande wa magaribi wa muji wa Ai, kati ya muji wa Ai na Beteli. Lakini Yoshua akalala usiku huo katika kambi ya Waisraeli.