Joshua 9:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafalme wote waliokuwa ngambo ya mto Yordani katika nchi ya milimani na kwenye tambarare na eneo lote la pwani ya bahari ya Mediteranea kuelekea Lebanoni, Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, waliposikia habari za Waisraeli,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi mwa Yordani waliposikia haya yote, na wale waliokuwa katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika pwani yote ya Bahari Kuu hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi),
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafalme wote waliokuwa ng'ambo ya mto Yordani katika nchi ya milimani na kwenye tambarare na eneo lote la pwani ya bahari ya Mediteranea kuelekea Lebanoni, Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, waliposikia habari za Waisraeli,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi ya Yordani waliposikia juu ya haya yote, wale waliokuwa katika nchi ya vilima, upande wa magharibi mwa vilima na katika pwani yote ya hiyo Bahari Kuu, hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi),
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ikawa wafalme wote waliokuwa magharibi mwa Yordani waliposikia juu ya haya yote, wale waliokuwa katika nchi ya vilima, upande wa magharibi mwa vilima na katika pwani yote ya hiyo Bahari Kuu, hadi kufikia Lebanoni (wafalme wa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi),
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari za mambo hayo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafalme wote waliokuwa ngambo ya mto Yordani katika nchi ya milimani na kwenye tambarare na eneo lote la pwani ya bahari ya Mediteranea kuelekea Lebanoni, Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, waliposikia habari za Waisraeli,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipoyasikia hayo wafalme wote waliokaa ng'ambo ya huku ya Yordani milimani na katika nchi ya tambarare na huko pwani po pote penye Bahari Kubwa panapoelekea Libanoni. Wahiti na Waamori na Wakanaani na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng’ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafalme wote waliokuwa ngambo ya muto Yordani katika inchi ya milima na kwenye mabonde na eneo lote la pembeni ya bahari ya Mediteranea kuelekea Lebanoni, Wahiti, Waamori, Wakanana, Waperizi, Wahivi na Wayebusi waliposikia habari za Waisraeli,