Joshua 9:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamjibu Yoshua, “Tuliambiwa kwamba kwa hakika Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alimwamuru mtumishi wake Mose awaangamize wakazi wote wa nchi hii na kuwapa nyinyi nchi hii iwe mali yenu. Kwa hivyo, tulihofia maisha yetu na ndipo tukafanya jambo hili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjibu Yoshua, “Watumwa wako waliambiwa waziwazi jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote na kuwaangamiza wakazi wake wote toka mbele zenu. Kwa hiyo tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, ndiyo maana tukafanya neno hili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo Bwana, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamjibu Yoshua, “Tuliambiwa kwamba kwa hakika Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alimwamuru mtumishi wake Mose awaangamize wakazi wote wa nchi hii na kuwapa nyinyi nchi hii iwe mali yenu. Kwa hivyo, tulihofia maisha yetu na ndipo tukafanya jambo hili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjibu Yoshua, “Watumwa wako waliambiwa waziwazi jinsi BWANA Mungu wenu alivyomwamuru mtumishi wake Mose kuwapa ninyi nchi hii yote na kuwafutilia mbali wakazi wake wote mbele zenu. Kwa hiyo tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, ndiyo maana tukafanya neno hili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjibu Yoshua, “Watumwa wako waliambiwa waziwazi jinsi bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote na kuwaangamiza wakazi wake wote toka mbele zenu. Kwa hiyo tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, ndiyo maana tukafanya neno hili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo BWANA, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele yenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamjibu Yoshua, “Tuliambiwa kwamba kwa hakika Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alimwamuru mtumishi wake Mose awaangamize wakazi wote wa nchi hii na kuwapa nyinyi nchi hii iwe mali yenu. Kwa hivyo, tulihofia maisha yetu na ndipo tukafanya jambo hili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakamjibu Yosua wakisema: Watumwa wako walipashwa habari za kwamba: Bwana Mungu wako alimwagiza mtumishi wake Mose kuwapa ninyi nchi hii yote nzima, mwangamize wenyeji wote wa nchi hii, watoweke mbele yenu. Kwa hiyo tukaingiwa na oga mwingi rohoni mwetu wa kuwaogopa ninyi, kwa hiyo tukalifanya jambo lile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo BWANA, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamujibu Yoshua: “Tuliambiwa kwamba kwa hakika Yawe, Mungu wenu, alimwamuru mutumishi wake Musa awaangamize wakaaji wote wa inchi hii na kuwapa ninyi inchi hii ikuwe mali yenu. Kwa hivyo, tuliogopea maisha yetu na ndipo tukafanya jambo hili.