Joshua 9:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamjibu, “Sisi, watumishi wako, tumetoka nchi ya mbali na tumekuja kwa maana tumesikia sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; tulipata habari za umaarufu wake na yote aliyoyafanya nchini Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao wakamjibu: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya umaarufu wa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Kwa kuwa tumesikia taarifa zake: hayo yote aliyofanya huko Misri,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako twatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la Bwana, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamjibu, “Sisi, watumishi wako, tumetoka nchi ya mbali na tumekuja kwa maana tumesikia sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; tulipata habari za umaarufu wake na yote aliyoyafanya nchini Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao wakamjibu: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya umaarufu wa BWANA Mungu wenu. Kwa kuwa tumesikia taarifa zake: hayo yote aliyofanya huko Misri,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao wakamjibu: “Watumishi wako wametoka nchi ya mbali sana kwa ajili ya umaarufu wa bwana Mwenyezi Mungu wenu. Kwa kuwa tumesikia taarifa zake: hayo yote aliyofanya huko Misri,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako tunatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la BWANA, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari za hayo yote aliyoyafanya huko Misri,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamjibu, “Sisi, watumishi wako, tumetoka nchi ya mbali na tumekuja kwa maana tumesikia sifa za jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; tulipata habari za umaarufu wake na yote aliyoyafanya nchini Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamwambia: Watumwa wako wametoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wako, kwani tumeusikia uvumi wake nayo yote, aliyoyafanya huko Misri,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako twatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la BWANA, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamujibu: “Sisi, watumishi wako, tumetoka inchi ya mbali na tumekuja kwa maana tumesikia sifa za jina la Yawe, Mungu wenu. Tulipata habari za utukufu wake na yote aliyoyafanya katika inchi ya Misri.