Jude 1:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu hao ni kama mawimbi makali ya bahari, na matendo yao ya aibu yanatoka kama povu. Wao ni kama nyota zinazotangatanga ambazo zimewekewa milele mahali pa giza kuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wao ni mawimbi makali ya bahari, yakitoa povu la aibu yao wenyewe, ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba waliowekewa milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kama mapovu machafu juu ya mawimbi ya bahari, kila mtu anaweza kuona mambo ya aibu wanayoyafanya. Ni kama nyota zinazotangatanga angani. Nao wameandaliwa mahali penye giza kuu milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu hao ni kama mawimbi makali ya bahari, na matendo yao ya aibu yanaonekana dhahiri kama vile mapovu ya mawimbi. Wao ni kama nyota zinazotangatanga, ambao Mungu amewawekea mahali pao milele katika giza kuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu hao ni kama mawimbi makali ya bahari, na matendo yao ya aibu yanatoka kama povu. Wao ni kama nyota zinazotangatanga ambazo zimewekewa milele mahali pa giza kuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao ni mawimbi makali ya bahari, yakitoa povu la aibu yao wenyewe, ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao ni mawimbi makali ya bahari, yakitoa povu la aibu yao wenyewe, ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba waliowekewa milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu hao ni kama mawimbi makali ya bahari, na matendo yao ya aibu yanatoka kama povu. Wao ni kama nyota zinazotangatanga ambazo zimewekewa milele mahali pa giza kuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena huwa kama mawimbi makali ya bahari yanayoyatoa mambo yao yaliyo yenye soni kuwa kama mapovu, huwa kama nyota zipoteazo ovyo, ambazo fungu lao, walilowekewa, ni lile giza jingi lililoko kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafanana na zoruba kubwa ya bahari na matendo yao ya haya yanaonekana kama pofu ya zoruba. Wanafanana vilevile na nyota zinazotangatanga; Mungu amekwisha kuwawekea nafasi katika giza kubwa kwa milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ni mawimbi ya bahari vasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu, ni nyota zipoteazo, ambao giza ndio akiba yao waliowekewa milele.