Jude 1:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao ndio wanaosababisha mafarakano, watu wa fikira za kidunia, wasio na Roho wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa ndio watu wanaowagawanya ninyi, wanaofuata tamaa zao za asili, wala hawana Roho wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hawa ni watu wanaowagawa katika makundi. Si wa rohoni kwa sababu hawana Roho Mtakatifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hao ndio watu wanaosababisha mafarakano, watu wanaotawaliwa na tamaa zao za kidunia, watu wasio na Roho wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao ndio wanaosababisha mafarakano, watu wa fikira za kidunia, wasio na Roho wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio watu wanaowagawa ninyi, wafuatao tamaa zao za asili, wala hawana Roho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio watu wanaowagawa ninyi, wafuatao tamaa zao za asili, wala hawana Roho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu hao ndio waletao utengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao ndio wanaosababisha mafarakano, watu wa fikira za kidunia, wasio na Roho wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao ndio wanaoleta matengano, ni wa kimtu tu, lakini Roho hawanayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu hao ndio waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu hawa ndio wanaoleta matengano; wanatawaliwa na tabia za kimwili nao hawana Roho wa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Watu hawo ndio wajitengao, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.