Jude 1:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nyinyi, wapenzi wangu, jijengeni wenyewe juu ya imani yenu takatifu kabisa. Salini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninyi wapendwa, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ninyi, rafiki wapendwa, itumieni imani yenu takatifu zaidi kusaidiana ninyi kwa ninyi ili muwe imara zaidi katika imani. Ombeni kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ninyi, wapenzi wangu, endeleeni kujijenga kikamilifu katika imani yenu takatifu. Salini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nyinyi, wapenzi wangu, jijengeni wenyewe juu ya imani yenu takatifu kabisa. Salini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninyi wapenzi, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho Mtakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ninyi wapendwa, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nyinyi, wapenzi wangu, jijengeni wenyewe juu ya imani yenu takatifu kabisa. Salini kwa nguvu ya Roho Mtakatifu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi, wapendwa, jijengeni wenyewe mkiyatumia mategemeo yenu matakatifu kuwa msingi! Mwombeni Mungu kwa nguvu ya Roho takatifu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi wapendwa wangu, muendelee kusimama imara katika imani yenu inayokuwa takatifu sana, mukiomba kwa uwezo wa Roho Mutakatifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imaui yenu iliyo takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu,