Jude 1:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
waokoeni kwa kuwanyakua kutoka motoni. Lakini kwa wengine muwe na huruma pamoja na tahadhari, mkichukia hata mavazi yao yenye madoa ya tamaa zao mbaya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
okoeni wengine kwa kuwanyakua kutoka motoni; nao wengine wahurumieni mkiwa na hofu, mkichukia hata vazi lenye mawaa na kutiwa unajisi na mwili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waokoeni wale wanaoishi katika hatari ya moto wa jehanamu. Muwatendee wengine kwa rehema, lakini muwe waangalifu kuwa maisha yao maovu yasichafue mwenendo wenu mwema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
waokoeni kwa kuwanyakua kutoka motoni; na kwa wengine muwe na huruma pamoja na hofu, lakini chukieni hata mavazi yao ambayo yamechafuliwa na tamaa zao mbaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
waokoeni kwa kuwanyakua kutoka motoni. Lakini kwa wengine muwe na huruma pamoja na tahadhari, mkichukia hata mavazi yao yenye madoa ya tamaa zao mbaya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wengine waokoeni kwa kuwanyakua kutoka kwenye moto; nao wengine wahurumieni mkiwa na hofu, mkichukia hata vazi lenye mawaa na kutiwa unajisi na mwili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wengine waokoeni kwa kuwanyakua kutoka kwenye moto; nao wengine wahurumieni mkiwa na hofu, mkichukia hata vazi lenye mawaa na kutiwa unajisi na mwili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
waokoeni kwa kuwanyakua kutoka motoni. Lakini kwa wengine muwe na huruma pamoja na tahadhari, mkichukia hata mavazi yao yenye madoa ya tamaa zao mbaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waokoeni mkiwapokonya motoni! Lakini wako na wengine, mwahurumie kwa kuogopa! Sharti mchukizwe nazo nguo zao zilizochafuliwa na miili yao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
muwaokoe, mukiwaopoa toka katika moto. Muwasikilie vilevile wengine huruma, lakini kwa woga, mukichukia hata nguo zao zilizochafuliwa na tamaa zao mbaya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali wengine waokoeni kwa khofu, mkiwanyakua katika moto, mkilichukia hatta vazi lililotiwa takataka na mwili.