Jude 1:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa nataka kuwakumbusheni mambo fulani, ingawaje haya mlikwisha fahamishwa kikamilifu mara moja: Kumbukeni jinsi Bwana alivyowaokoa watu wa Israeli na kuwatoa katika nchi ya Misri, lakini baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa mmekwisha kujua haya yote, nataka niwakumbushe kuwa Mwenyezi Mungu, akiisha kuwaokoa watu wake kutoka nchi ya Misri, baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninataka kuwasaidia mkumbuke baadhi ya vitu mnavyovifahamu tayari: Kumbukeni kwamba Bwana aliwaokoa watu wake kwa kuwatoa katika nchi ya Misri. Lakini baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nataka kuwakumbusheni mambo fulani ambayo mmekwisha yajua: kumbukeni jinsi Bwana alivyowaokoa watu wa Israeli na kuwatoa katika nchi ya Misri, lakini baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa nataka kuwakumbusheni mambo fulani, ingawaje haya mlikwisha fahamishwa kikamilifu mara moja: kumbukeni jinsi Bwana alivyowaokoa watu wa Israeli na kuwatoa katika nchi ya Misri, lakini baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa mmekwisha kujua haya yote, nataka niwakumbushe kuwa Bwana akiisha kuwaokoa watu wake kutoka Misri, baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa mmekwisha kujua haya yote, nataka niwakumbushe kuwa Mwenyezi Mungu akiisha kuwaokoa watu wake kutoka nchi ya Misri, baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa nataka kuwakumbusheni mambo fulani, ingawaje haya mlikwisha fahamishwa kikamilifu mara moja: Kumbukeni jinsi Bwana alivyowaokoa watu wa Israeli na kuwatoa katika nchi ya Misri, lakini baadaye aliwaangamiza wale ambao hawakuamini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nataka kuwakumbusha ninyi mliokwisha kuyajua hayo yote: Yeye Bwana aliyewaokoa wao wa ukoo wetu katika nchi ya Misri ndiye aliyewaangamiza waliokataa kumtegemea tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ijapokuwa mumekwisha kujua kabisa mambo haya yote, ninataka kuwakumbusha namna Bwana alivyowaokoa Waisraeli kutoka katika inchi ya Misri, lakini kisha, akawaangamiza wale waliokataa kuamini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena napenda kuwakumbusha, ijapo mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, baada ya kuwaokoa watu katika inchi ya Misri, aliwaharibu wasioamini.