Jude 1:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na, malaika ambao hawakuridhika na cheo chao, wakayaacha makao yao ya asili, Mungu amewafunga gizani kwa minyororo ya milele wahukumiwe siku ile kuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao malaika ambao hawakulinda nafasi zao, lakini wakayaacha makao yao, hawa amewaweka katika giza, wakiwa wamefungwa kwa minyororo ya milele kwa ajili ya hukumu Siku ile kuu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kumbukeni malaika waliopoteza mamlaka yao ya kutawala. Waliacha mahali pao pa kuishi. Hivyo Bwana amewaweka gizani, wamefungwa kwa minyororo ya milele, mpaka watakapohukumiwa siku iliyo kuu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na, malaika ambao hawakuridhika na cheo chao, wakayaacha makao yao ya asili, Mungu amewafunga gizani kwa minyororo ya milele wahukumiwe Siku ile kuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na, malaika ambao hawakuridhika na cheo chao, wakayaacha makao yao ya asili, Mungu amewafunga gizani kwa minyororo ya milele wahukumiwe siku ile kuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao malaika ambao hawakulinda nafasi zao, lakini wakayaacha makao yaliyokuwa yao hasa, hawa amewaweka katika giza, wakiwa wamefungwa kwa minyororo ya milele kwa ajili ya hukumu siku ile kuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao malaika ambao hawakulinda nafasi zao, lakini wakayaacha makao yao, hawa amewaweka katika giza, wakiwa wamefungwa kwa minyororo ya milele kwa ajili ya hukumu Siku ile kuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na, malaika ambao hawakuridhika na cheo chao, wakayaacha makao yao ya asili, Mungu amewafunga gizani kwa minyororo ya milele wahukumiwe siku ile kuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata malaika, wasioulinda ukuu wao wakijiendea na kuyaacha makao yao, amewafunga penye giza kwa mapingu yasiyovunjika, waingoje ile siku kubwa, wahukumiwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukumbuke vilevile wamalaika wale waliokosa kulinda vema cheo chao, lakini wakaacha makao yao: Mungu akawaweka katika nafasi ya giza, wakifungwa minyororo ya milele kwa kungojea Siku ile ya hukumu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.