Jude 1:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo ndivyo pia walivyo watu hawa. Ndoto zao huwaongoza katika kuichafua miili yao wenyewe, kuyadharau mamlaka ya Mungu na kuvitukana viumbe vitukufu vya huko juu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo, hawa waotao ndoto huutia mwili unajisi, hukataa kuwa chini ya mamlaka na kunena mabaya juu ya wenye mamlaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni sawasawa na watu hawa waliojiingiza kwenye kundi lenu. Wanaongozwa na ndoto, wanajichafua wenyewe kwa dhambi. Wanapuuza mamlaka ya Bwana na kusema mambo mabaya kinyume na walio watukufu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo ndivyo pia walivyo watu hawa. ndoto zao huwaongoza katika kuichafua miili yao wenyewe, kuyadharau mamlaka ya Mungu na kuvitukana viumbe vitukufu vya huko juu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo ndivyo pia walivyo watu hawa. Ndoto zao huwaongoza katika kuichafua miili yao wenyewe, kuyadharau mamlaka ya Mungu na kuvitukana viumbe vitukufu vya huko juu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo, hawa waotao ndoto huutia mwili unajisi, hukataa kuwa chini ya mamlaka na kunena mabaya juu ya wenye mamlaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo, hawa waotao ndoto huutia mwili unajisi, hukataa kuwa chini ya mamlaka na kunena mabaya juu ya wenye mamlaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo ndivyo pia walivyo watu hawa. Ndoto zao huwaongoza katika kuichafua miili yao wenyewe, kuyadharau mamlaka ya Mungu na kuvitukana viumbe vitukufu vya huko juu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, wale wanavyofanana navyo, wako kama wenye ndoto, huichafua miili yao, huutangua ukuu, huwatukana wenye utukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata hivi, watu hawa vilevile wanafanana nao; maono yao yanawasukuma kuchafua miili yao na kuzarau mamlaka ya Mungu na kutukana viumbe vitukufu vya mbinguni.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, hutukana matukufu.