Judges 1:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akamjibu, “Nipe zawadi! Naomba unipe chemchemi za maji kwani eneo ulilonipa huko Negebu ni kavu.” Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Ndipo Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa wewe umeniweka katika nchi ya Negebu, basi unipe na vijito vya maji pia. Kalebu akampa vile vijito vya maji vya juu na vijito vya chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akamjibu, “Nipe zawadi! Naomba unipe chemchemi za maji kwani eneo ulilonipa huko Negebu ni kavu.” Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akajibu, “Naomba unifanyie upendeleo maalum. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Ndipo akampa chemchemi za juu na za chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Ndipo Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa wewe umeniweka katika nchi ya Negebu, basi unipe na vijito vya maji pia. Kalebu akampa vile vijito vya maji vya juu na vijito vya chini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akamjibu, “Nipe zawadi! Naomba unipe chemchemi za maji kwani eneo ulilonipa huko Negebu ni kavu.” Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akamwambia: Nipe tunzo la kunibariki! Kwa kuwa umenipeleka katika nchi ya kusini, nipe nazo mboji za maji! Ndipo, Kalebu alipompa zile mboji zilizokuwa upande wa juu, nazo zilizokuwa upande wa chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa wewe umeniweka katika nchi ya Negebu, basi unipe na vijito vya maji pia. Kalebu akampa vile vijito vya maji vya juu na vijito vya chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamujibu: “Unipe zawadi! Ninaomba unipe chemichemi za maji maana kule upande wa kusini ni jangwa.” Kalebu akamupa chemichemi za upande wa juu na za chini.