Judges 1:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa kabila la Manase hawakuwafukuza wakazi wa miji ya Beth-sheani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Dori na vijiji vyake, Ibleamu na vijiji vyake, na Megido pamoja na vijiji vyake. Wakanaani waliendelea kukaa huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Manase hawakuwafukuza watu wa Beth-Shani na makazi yake, au watu wa Taanaki na makazi yake, au watu wa Dori na makazi yake, au watu wa Ibleamu na makazi yake, au watu wa Megido na makazi yake, kwa kuwa Wakanaani walikuwa wameamua kuishi katika nchi ile.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Bethsheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa kabila la Manase hawakuwafukuza wakazi wa miji ya Beth-sheani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Dori na vijiji vyake, Ibleamu na vijiji vyake, na Megido pamoja na vijiji vyake. Wakanaani waliendelea kukaa huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Manase hawakuwafukuza watu wa Beth-Shani na vijiji vyake, au watu wa Taanaki na vijiji vyake, au watu wa Dori na vijiji vyake, au watu wa Ibleamu na vijiji vyake, au watu wa Megido na vijiji vyake, lakini Wakanaani waliazimu kuishi katika nchi ile.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Manase hawakuwafukuza watu wa Beth-Shani na vijiji vyake, au watu wa Taanaki na vijiji vyake, au watu wa Dori na vijiji vyake, au watu wa Ibleamu na vijiji vyake, au watu wa Megido na vijiji vyake, lakini Wakanaani waliazimu kuishi katika nchi ile.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Beth-sheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa kabila la Manase hawakuwafukuza wakazi wa miji ya Beth-sheani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Dori na vijiji vyake, Ibleamu na vijiji vyake, na Megido pamoja na vijiji vyake. Wakanaani waliendelea kukaa huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wamanase hawakuwafukuza wenyeji wa Beti-Seani na wa mitaa yake, wala wa Taanaki na wa mitaa yake, wala wa Dori na wa mitaa yake, wala wenyeji wa Ibileamu na wa mitaa yake, wala wenyeji wa Megido na wa mitaa yake. Ndivyo, Wakanaani walivyopata kukaa kwanza katika nchi hii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Manase hakuwatoa wenyeji wa Bethsheani na miji yake, wala hao waliokaa Taanaki na miji yake, wala hao waliokaa Dori na miji yake, wala hao waliokaa Ibleamu na miji yake, wala hao waliokaa Megido na miji yake; lakini hao Wakanaani walikuwa hawakukubali kuiacha nchi hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa kabila la Manase hawakuwafukuza wakaaji wa miji ya Beti-Seani na vijiji vyake, Tanaki na vijiji vyake, Dori na vijiji vyake, Ibileamu na vijiji vyake, na Megido pamoja na vijiji vyake. Wakanana waliendelea kukaa kule.