Judges 1:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa kabila la Yuda wakawaambia ndugu zao, watu wa kabila la Simeoni, “Shirikianeni nasi tunapokwenda kuitwaa nchi hiyo ambayo tumepewa. Nasi, pia tutashirikiana nanyi kwenda kuitwaa nchi mtakayopewa.” Hivyo kabila la Simeoni likakubali kushirikiana nao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wanaume wa Yuda wakawaambia Wasimeoni ndugu zao, “Pandeni pamoja nasi katika nchi tuliyopewa, ili tupate kupigana na Wakanaani. Sisi pia tutaenda pamoja nanyi katika sehemu yenu mliyopewa.” Basi Wasimeoni wakaenda pamoja nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika kura yangu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika kura yako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa kabila la Yuda wakawaambia ndugu zao, watu wa kabila la Simeoni, “Shirikianeni nasi tunapokwenda kuitwaa nchi hiyo ambayo tumepewa. Nasi, pia tutashirikiana nanyi kwenda kuitwaa nchi mtakayopewa.” Hivyo kabila la Simeoni likakubali kushirikiana nao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo watu wa Yuda wakawaambia Wasimeoni ndugu zao, “Pandeni pamoja nasi katika nchi tuliyopewa, ili tupate kupigana na Wakanaani. Sisi pia tutakwenda pamoja nanyi katika sehemu yenu mliyopewa.” Basi Wasimeoni wakaenda pamoja nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo watu wa Yuda wakawaambia Wasimeoni ndugu zao, “Pandeni pamoja nasi katika nchi tuliyopewa, ili tupate kupigana na Wakanaani. Sisi pia tutakwenda pamoja nanyi katika sehemu yenu mliyopewa.” Basi Wasimeoni wakaenda pamoja nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika eneo langu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika eneo lako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa kabila la Yuda wakawaambia ndugu zao, watu wa kabila la Simeoni, “Shirikianeni nasi tunapokwenda kuitwaa nchi hiyo ambayo tumepewa. Nasi, pia tutashirikiana nanyi kwenda kuitwaa nchi mtakayopewa.” Hivyo kabila la Simeoni likakubali kushirikiana nao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yuda alipomwambia ndugu yake Simeoni: Panda pamoja nami katika nchi hiyo, niliyoipata kwa kura, tupigane na Wakanaani! Kisha nami nitapanda na wewe katika nchi, uliyoipata wewe kwa kura. Kwa hiyo Simeoni akaenda naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika kura yangu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika kura yako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa kabila la Yuda wakawaambia wandugu zao, watu wa kabila la Simeoni: “Mushirikiane nasi tunapokwenda kuitwaa inchi hiyo ambayo tumepewa. Nasi, vilevile tutashirikiana nanyi kwenda kuitwaa inchi mutakayopewa.” Hivyo kabila la Simeoni likakubali kushirikiana nao.