Judges 1:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waamori pia walikuwa wameamua kuendelea kuishi katika Mlima Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu; lakini nguvu ya nyumba ya Yusufu ilipoongezeka, wao pia wakashindwa na wakalazimika kuingia katika kazi ya kulazimishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waamori pia wakaendelea kukaa katika Mlima Heresi, katika Aiyaloni na Shaalbimu, lakini mkono wa nyumba ya Yosefu ukawalemea, nao wakashindwa hata wakalazimika kuingia katika kazi ya kulazimishwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waamori pia wakaendelea kukaa katika Mlima Heresi, katika Aiyaloni na Shaalbimu, lakini mkono wa nyumba ya Yusufu ukawalemea, nao wakashindwa hata wakalazimika kuingia katika kazi ya kulazimishwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Waamori walivyopata kukaa kwanza mlimani kwa Heresi na Ayaloni na Salabimu; lakini mikono yao wa mlango wa Yosefu ilipowalemea, wakawatumikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Ayaloni na Salabimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efuraimu waliwatawala Waamori na kuwatumikisha kazi za kulazimishwa.