Judges 1:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Adoni-bezeki akasema, “Wafalme sabini waliokatwa vidole gumba vya mikono na miguu waliokota makombo chini ya meza yangu. Sasa Mungu amenilipa kama nilivyotenda.” Wakampeleka Yerusalemu, akafia huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Adoni-Bezeki akasema, “Wafalme sabini waliokuwa wamekatwa vidole vyao vya gumba vya mikono na vya miguu walikuwa wakiokota makombo chini ya meza yangu. Sasa Mungu amenilipa haya kwa yale niliyowatendea.” Wakamleta Yerusalemu, naye akafa huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vyanda vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Adoni-bezeki akasema, “Wafalme sabini waliokatwa vidole gumba vya mikono na miguu waliokota makombo chini ya meza yangu. Sasa Mungu amenilipa kama nilivyotenda.” Wakampeleka Yerusalemu, akafia huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Adoni-Bezeki akasema, “Nimewatendea wafalme sabini kama nilivyotendewa na kuwalisha makombo ya chakula chini ya meza yangu. Sasa Mungu amenilipa haya, kama yale niliyowatendea.” Wakamleta Yerusalemu, naye akafa huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Adoni-Bezeki akasema, “Nimewatendea wafalme sabini kama nilivyotendewa na kuwalisha makombo ya chakula chini ya meza yangu. Sasa Mungu amenilipa haya, kama yale niliyowatendea.” Wakamleta Yerusalemu, naye akafa huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vidole gumba vyao, vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo hivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Adoni-bezeki akasema, “Wafalme sabini waliokatwa vidole gumba vya mikono na miguu waliokota makombo chini ya meza yangu. Sasa Mungu amenilipa kama nilivyotenda.” Wakampeleka Yerusalemu, akafia huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Adoni-Bezeki akasema: Wafalme 70 waliokatwa vidole gumba vya mikono na vya miguu walikuwa wakiokota vyakula vyao chini ya meza yangu, kama nilivyofanya, ndivyo, Mungu alivyonilipisha, kisha wakampeleka Yerusalemu, akafa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vyanda vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Adoni-Bezeki akasema: “Wafalme makumi saba waliokatwa vidole gumba vya mikono na miguu waliokota makombo chini ya meza yangu. Sasa Mungu amenilipa kama nilivyotenda.” Wakamupeleka Yerusalema, akakufia kule.