Judges 1:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, watu wa kabila la Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani walioishi kwenye nchi ya milima, Negebu na kwenye nchi tambarare.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya hayo, watu wa Yuda wakateremka kupigana na Wakanaani walioishi katika nchi ya vilima, na Negebu, na nchi ya Shefela.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baadaye wana wa Yuda wakatelemka ili wapigane na hao Wakanaani waliokaa katika nchi ya milimani, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, watu wa kabila la Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani walioishi kwenye nchi ya milima, Negebu na kwenye nchi tambarare.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya hayo, watu wa Yuda wakatelemka kupigana na Wakanaani walioishi katika nchi ya vilima, yaani, Negebu na nchi chini ya vilima vya magharibi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya hayo, watu wa Yuda wakateremka kupigana na Wakanaani walioishi katika nchi ya vilima, yaani, Negebu na nchi chini ya vilima vya magharibi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baadaye wana wa Yuda wakateremka ili wapigane na hao Wakanaani waliokaa katika nchi yenye milima, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye, watu wa kabila la Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani walioishi kwenye nchi ya milima, Negebu na kwenye nchi tambarare.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baadaye wana wa Yuda wakashuka kupigana na Wakanaani waliokaa milimani na kusini na katika nchi ya tambarare.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baadaye wana wa Yuda wakatelemka ili wapigane na hao Wakanaani waliokaa katika nchi ya milimani, na nchi ya Negebu, na nchi ya Shefela.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, watu wa kabila la Yuda wakakwenda kupigana na Wakanana walioishi kwenye inchi ya milima, Negebu na kwenye inchi ya bonde.