Judges 10:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli walitenda tena uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu wakatumikia Mabaali, Maashtarothi, na miungu ya Shamu, ya Sidoni, ya Moabu, ya Amoni na ya Wafilisti. Walimwacha Mwenyezi-Mungu na wala hawakumwabudu tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tena Waisraeli wakatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, na miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni, na miungu ya Wafilisti. Na kwa kuwa Waisraeli walimwacha Mwenyezi Mungu wala hawakuendelea kumtumikia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamwacha Bwana, wala hawakumtumikia yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli walitenda tena uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu wakatumikia Mabaali, Maashtarothi, na miungu ya Shamu, ya Sidoni, ya Moabu, ya Amoni na ya Wafilisti. Walimwacha Mwenyezi-Mungu na wala hawakumwabudu tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wana wa Israeli wakatenda tena maovu machoni pa BWANA. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni na miungu ya Wafilisti. Kwa kuwa Waisraeli walimwacha BWANA wala hawakuendelea kumtumikia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wana wa Israeli wakatenda tena maovu machoni pa bwana. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni na miungu ya Wafilisti. Kwa kuwa Waisraeli walimwacha bwana wala hawakuendelea kumtumikia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamuacha BWANA, wala hawakumtumikia yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli walitenda tena uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu wakatumikia Mabaali, Maashtarothi, na miungu ya Shamu, ya Sidoni, ya Moabu, ya Amoni na ya Wafilisti. Walimwacha Mwenyezi-Mungu na wala hawakumwabudu tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wa Isiraeli walipoendelea kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, wakiyatumikia Mabaali na Maastaroti na miungu ya Ushami na miungu ya Sidoni na miungu ya Moabu na miungu ya wana wa Amoni na miungu ya Wafilisti, basi, walipomwacha Bwana hivyo, wasimtumikie,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamwacha BWANA, wala hawakumtumikia yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waisraeli wakatenda tena uovu mbele ya Yawe, wakatumikia Mabali, Mastaroti, na miungu ya Aramu, ya Sidona, ya Moabu, ya Amoni na ya Wafilistini. Wakamwacha Yawe wala hawakumwabudu tena.