Judges 11:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeftha akapeleka ujumbe kwa mfalme wa Amoni akamwambia, “Una ugomvi gani nasi hata uje kuishambulia nchi yetu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yefta akatuma wajumbe kwa mfalme wa Waamoni akisema, “Una nini nasi, hata umekuja kushambulia nchi yetu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yeftha akatuma wajumbe waende kwa mfalme wa wana wa Amoni akasema, Je! Wewe una nini nami, hata umenijilia kupigana juu ya nchi yangu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeftha akapeleka ujumbe kwa mfalme wa Amoni akamwambia, “Una ugomvi gani nasi hata uje kuishambulia nchi yetu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yefta akatuma wajumbe kwa mfalme wa Waamoni akisema, “Una nini juu yetu, hata umekuja kushambulia nchi yetu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yefta akatuma wajumbe kwa mfalme wa Waamoni akisema, “Una nini juu yetu, hata umekuja kushambulia nchi yetu?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yeftha akatuma wajumbe waende kwa mfalme wa wana wa Amoni akasema, Je! Wewe una nini nami, hata umenijia kupigana juu ya nchi yangu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeftha akapeleka ujumbe kwa mfalme wa Amoni akamwambia, “Una ugomvi gani nasi hata uje kuishambulia nchi yetu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yefuta akatuma wajumbe kwa mfalme wa wana wa Amoni kwamba: Tuko na mapitano gani mimi na wewe, ukinijia kupiga vita katika nchi yangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yeftha akatuma wajumbe waende kwa mfalme wa wana wa Amoni akasema, Je! Wewe una nini nami, hata umenijilia kupigana juu ya nchi yangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yefuta akapeleka ujumbe kwa mufalme wa Amoni akamwambia: “Kuna maneno gani kati yako nasi hata ukuje kuishambulia inchi yetu?”