Judges 11:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme wa Amoni akawajibu hao wajumbe, “Waisraeli walipotoka Misri, walichukua nchi yangu kutoka mto Arnoni hadi mto Yaboki na mto Yordani. Sasa nirudishie nchi hiyo kwa amani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme wa Waamoni akawajibu wajumbe wale wa Yefta, “Waisraeli walipopanda kutoka Misri, waliichukua nchi yangu kuanzia Mto Arnoni hadi Mto Yaboki, hadi kufikia Mto Yordani. Sasa irudishe kwa amani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu hao wajumbe wa Yeftha Kwa sababu Israeli waliitwaa nchi yangu, hapo walipokwea kutoka katika nchi ya Misri, tokea Arnoni mpaka Yaboki, na hata Yordani; basi sasa rudisha hizo nchi tena pasipo matata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme wa Amoni akawajibu hao wajumbe, “Waisraeli walipotoka Misri, walichukua nchi yangu kutoka mto Arnoni hadi mto Yaboki na mto Yordani. Sasa nirudishie nchi hiyo kwa amani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme wa Waamoni akawajibu wajumbe wale wa Yefta, “Wakati Waisraeli walipopanda kutoka Misri, waliichukua nchi yangu kuanzia Arnoni mpaka Yaboki, hadi kufikia Yordani. Sasa rudisha kwa amani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme wa Waamoni akawajibu wajumbe wale wa Yefta, “Wakati Waisraeli walipopanda kutoka Misri, waliichukua nchi yangu kuanzia Arnoni mpaka Yaboki, hadi kufikia Yordani. Sasa rudisha kwa amani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu hao wajumbe wa Yeftha, “Kwa sababu Israeli waliitwaa nchi yangu, hapo walipokwea wakitoka katika nchi ya Misri, tokea Arnoni mpaka Yaboki, na hata Yordani; basi sasa rudisha hizo nchi tena kwa amani.”
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme wa Amoni akawajibu hao wajumbe, “Waisraeli walipotoka Misri, walichukua nchi yangu kutoka mto Arnoni hadi mto Yaboki na mto Yordani. Sasa nirudishie nchi hiyo kwa amani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu wajumbe wa Yefuta: Kwa kuwa Waisiraeli wameichukua nchi yangu kutoka Arnoni mpaka Yaboko na Yordani, walipotoka Misri kuja huku; sasa hizi nchi zirudishe pasipo kupiga vita!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu hao wajumbe wa Yeftha Kwa sababu Israeli waliitwaa nchi yangu, hapo walipokwea kutoka katika nchi ya Misri, tokea Arnoni mpaka Yaboki, na hata Yordani; basi sasa rudisha hizo nchi tena pasipo matata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme wa Amoni akawajibu hao wajumbe: “Waisraeli walipotoka Misri, walitwaa inchi yangu kutoka muto Arnoni mpaka kwenye muto Yaboki na muto Yordani. Sasa munirudishie inchi hiyo kwa amani.”