Judges 11:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Waisraeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu wakimwomba awaruhusu kupita katika nchi yake, lakini mfalme wa Edomu akakataa. Basi wakamwomba ruhusa mfalme wa Moabu naye pia akakataa. Kwa hiyo Waisraeli wakabaki Kadeshi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Waisraeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu, wakisema, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako.’ Lakini mfalme wa Edomu hakutusikia. Wakatuma wajumbe pia kwa mfalme wa Moabu, naye akakataa. Kwa hiyo Waisraeli wakakaa huko Kadeshi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo Israeli wakatuma wajumbe waende kwa mfalme wa Edomu, wakisema, Nakuomba sana unipe ruhusa nipite katika nchi yako; lakini mfalme wa Edomu hakusikia. Ni vivyo wakampelekea wajumbe mfalme wa Moabu; wala yeye hakukubali; basi Israeli wakakaa katika Kadeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Waisraeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu wakimwomba awaruhusu kupita katika nchi yake, lakini mfalme wa Edomu akakataa. Basi wakamwomba ruhusa mfalme wa Moabu naye pia akakataa. Kwa hiyo Waisraeli wakabaki Kadeshi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Israeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu, wakisema, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako,’ Lakini mfalme wa Edomu hakutusikia. Wakapeleka pia wajumbe kwa mfalme wa Moabu, naye akakataa. Kwa hiyo Israeli wakakaa huko Kadeshi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Israeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu, wakisema, ‘Tupe ruhusa kupita katika nchi yako,’ Lakini mfalme wa Edomu hakutusikia. Wakapeleka pia wajumbe kwa mfalme wa Moabu, naye akakataa. Kwa hiyo Israeli wakakaa huko Kadeshi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo Israeli wakatuma wajumbe waende kwa mfalme wa Edomu, wakisema, Nakuomba sana unipe ruhusa nipite katika nchi yako; lakini mfalme wa Edomu hakuwasikiliza. Pia waliwatuma wajumbe kwa mfalme wa Moabu; wala naye hakukubali; basi Israeli wakakaa katika Kadeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Waisraeli wakatuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu wakimwomba awaruhusu kupita katika nchi yake, lakini mfalme wa Edomu akakataa. Basi wakamwomba ruhusa mfalme wa Moabu naye pia akakataa. Kwa hiyo Waisraeli wakabaki Kadeshi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Waisiraeli walipotuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu kwamba: Na tupite katika nchi yako! Lakini mfalme wa Edomu hakuwasikia; naye mfalme wa Moabu akakataa, walipotuma kwake. Kwa hiyo Waisiraeli wakakaa kwanza Kadesi,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo Israeli wakatuma wajumbe waende kwa mfalme wa Edomu, wakisema, Nakuomba sana unipe ruhusa nipite katika nchi yako; lakini mfalme wa Edomu hakusikia. Ni vivyo wakampelekea wajumbe mfalme wa Moabu; wala yeye hakukubali; basi Israeli wakakaa katika Kadeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Waisraeli wakatuma wajumbe kwa mufalme wa Edomu wakimwomba awaruhusu kupita katika inchi yake, lakini mufalme wa Edomu akakataa. Basi wakamwomba mufalme wa Moabu ruhusa naye vilevile akakataa. Kwa hiyo Waisraeli wakabaki Kadesi.