Judges 11:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha wakasafiri wakipitia jangwani kuzunguka nchi ya Edomu na Moabu mpaka walipofika upande wa mashariki wa Moabu, wakapiga kambi ngambo ya mto Arnoni. Lakini hawakuingia eneo la Moabu. Mto Arnoni ndio uliokuwa mpaka wa Moabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Baadaye wakasafiri kupitia jangwa, wakiambaa na nchi za Edomu na Moabu, wakapitia upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, na kupiga kambi upande ule mwingine wa Mto Arnoni. Hawakuingia katika nchi ya Moabu, kwa kuwa Mto Arnoni ulikuwa mpaka wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, wakapanga marago upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha wakasafiri wakipitia jangwani kuzunguka nchi ya Edomu na Moabu mpaka walipofika upande wa mashariki wa Moabu, wakapiga kambi ng'ambo ya mto Arnoni. Lakini hawakuingia eneo la Moabu. Mto Arnoni ndio uliokuwa mpaka wa Moabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Baadaye wakasafiri kupitia katika jangwa wakiambaa-ambaa na hiyo nchi ya Edomu na Moabu, wakapitia upande wa mashariki wa nchi ya Moabu na kupiga kambi upande mwingine wa Arnoni. Hawakuingia katika nchi ya Moabu kwa kuwa Arnoni ilikuwa ndio mpaka wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Baadaye wakasafiri kupitia jangwa, wakiambaa na nchi za Edomu na Moabu, wakapitia upande wa mashariki wa nchi ya Moabu na kupiga kambi upande mwingine wa Arnoni. Hawakuingia katika nchi ya Moabu, kwa kuwa Arnoni ilikuwa mpaka wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki mwa nchi ya Moabu, wakapiga kambi upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha wakasafiri wakipitia jangwani kuzunguka nchi ya Edomu na Moabu mpaka walipofika upande wa mashariki wa Moabu, wakapiga kambi ngambo ya mto Arnoni. Lakini hawakuingia eneo la Moabu. Mto Arnoni ndio uliokuwa mpaka wa Moabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha wakapita nyikani na kuizunguka nchi ya Edomu na nchi ya Moabu. Walipoifikia nchi ya Moabu upande wa maawioni kwa jua wakapiga makambi ng'ambo ya Arnoni pasipo kuingia mipakani kwa Moabu, kwani Arnoni ndio mpaka wa Moabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, wakapanga marago upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wakasafiri wakipitia katika jangwa kuzunguka inchi ya Edomu na Moabu mpaka walipofika upande wa mashariki wa Moabu, wakapiga kambi ngambo ya muto Arnoni. Lakini hawakuingia katika eneo la Moabu. Muto Arnoni ndio uliokuwa mupaka wa Moabu.