Judges 11:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gileadi alikuwa pia na wana wengine kwa mke wake wa halali. Watoto wa mke huyo walipokuwa wakubwa, walimfukuza Yeftha kutoka nyumbani, wakamwambia, “Wewe huna haki ya kupata urithi kutoka kwa baba yetu, maana wewe ni mtoto wa mwanamke mwingine.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mke wa Gileadi pia akamzalia wana, nao walipokua, wakamfukuza Yefta, na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamii yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gileadi alikuwa pia na wana wengine kwa mke wake wa halali. Watoto wa mke huyo walipokuwa wakubwa, walimfukuza Yeftha kutoka nyumbani, wakamwambia, “Wewe huna haki ya kupata urithi kutoka kwa baba yetu, maana wewe ni mtoto wa mwanamke mwingine.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mke wa Gileadi akamzalia wana wengine, nao watoto hao walipokua, wakamfukuza Yefta na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamaa yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mke wa Gileadi akamzalia wana wengine, nao watoto hao walipokua, wakamfukuza Yefta na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamii yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya baba yetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gileadi alikuwa pia na wana wengine kwa mke wake wa halali. Watoto wa mke huyo walipokuwa wakubwa, walimfukuza Yeftha kutoka nyumbani, wakamwambia, “Wewe huna haki ya kupata urithi kutoka kwa baba yetu, maana wewe ni mtoto wa mwanamke mwingine.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mkewe Gileadi alikuwa amemzalia wana; hao wana wa huyu mwanamke walipokua wakamfukuza Yefuta wakimwambia: Haifai, ukipata urithi nyumbani mwa baba yetu, kwani wewe u mwana wa mwanamke mwingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gileadi alikuwa vilevile na wana wengine toka kwa muke wake. Watoto wa muke huyo walipokuwa wakubwa, wakamufukuza Yefuta kutoka kwao, wakamwambia: “Wewe hauna haki ya kupata urizi kutoka kwa baba yetu, maana wewe ni mutoto wa mwanamuke mwingine.”