Judges 11:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akajipatia ushindi mkubwa, akateka maeneo ishirini yaliyokuwa kati ya Aroeri, sehemu zilizozunguka Minithi na Abel-keramimu. Basi Waamoni wakashindwa kabisa na Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaharibu kabisa miji ishirini kuanzia Aroeri hadi karibu na Minithi, na kuendelea hadi Abel-Keramimu. Hivyo, Waisraeli wakawashinda Waamoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawapiga kutoka Aroeri hata kufikilia Minithi, miji ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa machinjo makuu mno. Basi hivyo wana wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akajipatia ushindi mkubwa, akateka maeneo ishirini yaliyokuwa kati ya Aroeri, sehemu zilizozunguka Minithi na Abel-keramimu. Basi Waamoni wakashindwa kabisa na Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawapiga kwa ushindi mkubwa kuanzia Aroeri mpaka karibu na Minithi na kuendelea mpaka Abel-Keramimu, miji yote iliyopigwa ni ishirini. Basi Israeli wakawashinda Waamoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawapiga kwa ushindi mkubwa kuanzia Aroeri mpaka karibu na Minithi na kuendelea mpaka Abel-Keramimu, miji yote iliyopigwa ni ishirini. Basi Israeli wakawashinda Waamoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawapiga kutoka Aroeri hadi kufikia Minithi, miji ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa pigo kuu mno. Basi hivyo wana wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akajipatia ushindi mkubwa, akateka maeneo ishirini yaliyokuwa kati ya Aroeri, sehemu zilizozunguka Minithi na Abel-keramimu. Basi Waamoni wakashindwa kabisa na Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawapiga kutoka Aroeri, mpaka mtu akifika Miniti kwenye miji ishirini hata Abeli-keramimu (Mbuga ya Mizabibu), pigo hilo likawa kubwa sana. Ndivyo, wana wa Amoni walivyonyenyekezwa mbele yao wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawapiga kutoka Aroeri hata kufikilia Minithi, miji ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa machinjo makuu mno. Basi hivyo wana wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akajipatia ushindi mukubwa, akateka maeneo makumi mbili yaliyokuwa kati ya Aroeri, sehemu zilizozunguka Miniti na Abeli-Keramimu. Basi Waamoni wakashindwa kabisa na Waisraeli.