Judges 11:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeftha alipokuwa anarudi nyumbani kwake huko Mizpa, binti yake akatoka kuja kumlaki akicheza na kupiga matari. Msichana huyo alikuwa ndiye mtoto wake wa pekee. Yeftha hakuwa na mtoto mwingine wa kiume wala wa kike.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yefta aliporudi nyumbani mwake huko Mispa, tazama, binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na kucheza. Alikuwa mwanawe wa pekee, hakuwa na mwana wala binti mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na machezo; naye alikuwa ni mwanawe pekee; hakuwa na mwingine, mwana wala binti, ila yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeftha alipokuwa anarudi nyumbani kwake huko Mizpa, binti yake akatoka kuja kumlaki akicheza na kupiga matari. Msichana huyo alikuwa ndiye mtoto wake wa pekee. Yeftha hakuwa na mtoto mwingine wa kiume wala wa kike.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yefta aliporudi nyumbani Mizpa, tazama, binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na kucheza. Alikuwa ndiye mtoto pekee, hakuwa na mwana wala binti mwingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yefta aliporudi nyumbani Mispa, tazama, binti yake akatoka ili kumlaki kwa matari na kucheza. Alikuwa ndiye mtoto pekee, hakuwa na mwana wala binti mwingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na akichezacheza; naye alikuwa ni mwanawe wa pekee; hakuwa na mwingine, wa kiume wala binti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeftha alipokuwa anarudi nyumbani kwake huko Mizpa, binti yake akatoka kuja kumlaki akicheza na kupiga matari. Msichana huyo alikuwa ndiye mtoto wake wa pekee. Yeftha hakuwa na mtoto mwingine wa kiume wala wa kike.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yefuta alipofika Misipa kwenye nyumba yake, mara mwanawe wa kike akatoka kumwendea njiani akipiga patu na kuchezacheza, naye alikuwa mwanawe wa pekee, kuliko yeye hakuwa na mwana mwingine, wala wa kiume, wala wa kike.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na machezo; naye alikuwa ni mwanawe pekee; hakuwa na mwingine, mwana wala binti, ila yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yefuta alipokuwa anarudi kwake kule Misipa, binti yake akatoka kuja kumupokea akicheza na kupiga matari. Binti huyo alikuwa ndiye mutoto wake wa pekee. Yefuta hakukuwa na mutoto mwingine mwanaume wala mwanamuke.