Judges 11:35 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeftha alipomwona, alirarua mavazi yake kwa huzuni na kusema, “O binti yangu! Umenivunja moyo. Wewe umekuwa chanzo kikubwa cha matatizo kwangu. Nimekwisha mwapia Mwenyezi-Mungu nami siwezi kuvunja kiapo changu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipomwona akararua mavazi yake akalia, “Ee! Binti yangu! Umenifanya niwe na huzuni na kunyong’onyea sana, kwa kuwa nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, ambayo siwezi kuivunja.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa alipomwona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia Bwana kinywa changu, nami siwezi kurejea nyuma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeftha alipomwona, alirarua mavazi yake kwa huzuni na kusema, “O binti yangu! Umenivunja moyo. Wewe umekuwa chanzo kikubwa cha matatizo kwangu. Nimekwisha mwapia Mwenyezi-Mungu nami siwezi kuvunja kiapo changu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipomwona akararua mavazi yake akalia, “Ee! Binti yangu! Umenifanya niwe na huzuni na kunyong'onyea sana, kwa kuwa nimeweka nadhiri kwa BWANA, ambayo siwezi kuivunja.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipomwona akararua mavazi yake akalia, “Ee! Binti yangu! Umenifanya niwe na huzuni na kunyong’onyea sana, kwa kuwa nimeweka nadhiri kwa bwana, ambayo siwezi kuivunja.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa alipomuona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurudi nyuma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeftha alipomwona, alirarua mavazi yake kwa huzuni na kusema, “O binti yangu! Umenivunja moyo. Wewe umekuwa chanzo kikubwa cha matatizo kwangu. Nimekwisha mwapia Mwenyezi-Mungu nami siwezi kuvunja kiapo changu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, alipomwona akazirarua nguo zake akilia: E mwanangu! Unaninyenyekeza sana! Kumbe wewe nawe u mmoja wao wanaonisikitisha! Mimi nimekifumbua kinywa changu kusema na Bwana, siwezi kuyarudisha niliyoyasema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa alipomwona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurejea nyuma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yefuta alipomwona, akapasua nguo yake kwa huzuni na kusema: “Ee binti yangu! Umenivunja moyo. Wewe umekuwa chanzo kikubwa cha matatizo kwangu. Nimekwisha kumwapia Yawe nami siwezi kuvunja kiapo changu.”