Judges 11:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yeftha akawaambia hao wazee wa Gileadi, “Je, si mlinichukia hata mkanifukuza kutoka kwa jamaa ya baba yangu? Kwa nini mnanijia sasa mkiwa katika taabu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yefta akawaambia viongozi wa Gileadi, “Je, si mlinichukia na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Kwa nini mwanijia sasa, wakati mko taabuni?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa wakati mlio katika taabu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yeftha akawaambia hao wazee wa Gileadi, “Je, si mlinichukia hata mkanifukuza kutoka kwa jamaa ya baba yangu? Kwa nini mnanijia sasa mkiwa katika taabu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yefta akawaambia, “Je, hamkunichukia mimi na kunifukuza katika nyumba ya baba yangu? Kwa nini mnanijia sasa, wakati mna matatizo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yefta akawaambia, “Je, hamkunichukia mimi na kunifukuza katika nyumba ya baba yangu? Kwa nini mnanijia sasa, wakati mna matatizo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Kwa nini basi mnanijia hivi sasa wakati mkiwa katika taabu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yeftha akawaambia hao wazee wa Gileadi, “Je, si mlinichukia hata mkanifukuza kutoka kwa jamaa ya baba yangu? Kwa nini mnanijia sasa mkiwa katika taabu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Yefuta akawaambia wazee wa Gileadi: Je? Ninyi ham wachukivu wangu? Hamkunifukuza nyumbani mwa baba yangu? Mbona sasa mnaposongwa mwanijia mimi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, Je! Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwani kunijilia hivi sasa wakati mlio katika taabu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yefuta akawaambia hao wazee wa Gileadi: “Si mulinichukia hata mukanifukuza kutoka kwa jamaa ya baba yangu? Kwa nini munanifikia sasa mukiwa katika taabu?”