Judges 12:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipoona kwamba hamkuja kuniokoa, nilikwenda, roho mkononi, kupigana na Waamoni, naye Mwenyezi-Mungu akawatia mikononi mwangu. Kwa nini sasa mnakuja kupigana na mimi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipoona kuwa hamniokoi, nikauhatarisha uhai wangu, nikavuka kupigana na Waamoni. Naye Mwenyezi Mungu akanipatia ushindi dhidi yao. Sasa kwa nini mnanijia leo ili kupigana nami?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nilipoona ya kuwa ninyi hamniokoi, niliuhatirisha uhai wangu, na kuvuka ili nipigane na wana wa Amoni, Bwana naye akawatia mkononi mwangu; basi kwa nini ninyi kunijia hivi leo kutaka kupigana nami?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipoona kwamba hamkuja kuniokoa, nilikwenda, roho mkononi, kupigana na Waamoni, naye Mwenyezi-Mungu akawatia mikononi mwangu. Kwa nini sasa mnakuja kupigana na mimi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipoona kuwa hamkunipa msaada nikauhatarisha uhai wangu na nikavuka kupigana na Waamoni. Naye BWANA akanipatia ushindi dhidi yao. Sasa kwa nini mnanijia leo ili kupigana nami?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipoona kuwa hamkunipa msaada nikauhatarisha uhai wangu na nikavuka kupigana na Waamoni. Naye bwana akanipatia ushindi dhidi yao. Sasa kwa nini mnanijia leo ili kupigana nami?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nilipoona ya kuwa ninyi hamniokoi, niliuhatarisha uhai wangu, na kuvuka ili nipigane na wana wa Amoni, BWANA naye akawatia mkononi mwangu; basi kwa nini ninyi kunijia hivi leo kutaka kupigana nami?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipoona kwamba hamkuja kuniokoa, nilikwenda, roho mkononi, kupigana na Waamoni, naye Mwenyezi-Mungu akawatia mikononi mwangu. Kwa nini sasa mnakuja kupigana na mimi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipoona, ya kuwa ninyi hamniokoi, nikajitoa mwenyewe, nikawaendea wana wa Amoni, naye Bwana akawatia mikononi mwangu Ni kwa sababu gani, mkinipandia leo hivi kupigana na mimi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nilipoona ya kuwa ninyi hamniokoi, niliuhatirisha uhai wangu, na kuvuka ili nipigane na wana wa Amoni, BWANA naye akawatia mkononi mwangu; basi kwa nini ninyi kunijia hivi leo kutaka kupigana nami?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipoona kwamba hamukukuja kuniokoa, nikahatarisha maisha yangu, nikavuka kwenda kupigana na Waamoni, naye Yawe akawatia katika mikono yangu. Kwa nini sasa munakuja kupigana na mimi?”